Kiungo mwenye kasi wa PSG, Angelo Di Maria amesema hatashangilia kama
atafanikiwa kufunga bao wakati wakivaa Real Madrid.
Di Maria ametua PSG akitokea Manchester United ambayo ilimnunua kutoka
Real Madrid ambayo sasa wako nayo kundi moja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Madrid itaanza kukutana na Madrid Oktoba 21 jijini Paris, Ufaranda
kabla ya kurudia Madrid Novemba 3.
“Nilipojua ninahamia PSG nilimueleza mke wangu hofu ya kwamba tunaweza
kupangwa na Real Madrid. Nilianza kujiuliza watanipokeaje siku nikienda pale na
timu nyingine.
“Tumekuwa pamoja, tulishinda makombe mengi kwa pamoja na walinionyesha
heshima kubwa. Mfano baada ya kujua ninaenda Manchester United, uwanja mzima walisimama
kuniaga.
“Ni watu walioonyesha upendo mkubwa kwangu, itakuwa vigumu kushangilia
kama nitafunga ingawa nitacheza kwa juhudi kubwa kwa ninataka mafanikio pia
nikiwa PSG, nataka kushinda makombe,” alisisitiza Di Maria.
0 maoni:
Post a Comment