Kampuni
ya StarTimes Media ya jijini Dar es salaam leo imeingia mkataba wa
udhamini na TFF kudhamini Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL)
inayoshirikisha timu 24 kutoka katika mikoa 16 ya Tanzania bara.
Akiongea na waandishi wa habari wakai uwekaji sahihi mkataba huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ameshukuru kituo cha Star Times kwa kuamua kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa kwenye chimbuko la vipaji na wachezaji wengie nchini.
Malinzi amesema udhamini huo wa shilingi milioni 900 kwa kipindi cha miaka mitatu, unatarajiwa kuongezeka wiki ijayo baada ya kuingia mkataba na mdhamini mwingine wa kurusha matangazo ya ligi hiyo kwa shilingi milioni 450 na kufikia jumla ya udhamini wa shilingi bilioni 1.3.

0 maoni:
Post a Comment