
3:50 AM

Unknown
Wachezaji
wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha
maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga.
Pamoja na Kidiaba
ambaye anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa
makalio, Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe
anayewania ubunge kupitia chama cha upinzani cha PND.
Nahodha huyo
wa Leopards mwenye umri wa miaka 39 amesema anaamini kuwa wachezaji
wanaweza kuwa viongozi bora na kuleta mabadiliko ya maendeleo katika
maeneo yao.
Uchaguzi
wa wabunge na urais utafanyika mwaka ujao nchini humo na ikiwa Kidiaba
atachaguliwa kuwa mbunge, bila shaka itakuwa ni historia katika mchezo
wa soka nchini humo.
Kidiaba alianza kuichezea timu ya taifa mwaka
2002 na ameshiriki katika michuano 11 ya kufuzu katika michuano ya kombe
la duniani na kwa ujumla kuichezea timu ya taifa mara 59.
Mwezi
Desemba, mwaka 2014 alitangaza kuwa alikuwa anajiuzulu baada ya
michuano ya mwaka huu ya mataifa bingwa barani Afrika lakini baadaye
akabadilisha mawazo ya kuendelea kucheza soka.
0 maoni:
Post a Comment