Tuesday, June 16, 2015

1
Jokate (kushoto) akizungumza katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni katibu mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous.
2
Mbunifu mkongwe wa mavazi nchini, Asia Idarous (kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni Katibu mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na msichana mwenye vipaji vingi, Jokate Mwegelo.
3
Katibu mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli (Katikati) akizungumza katika mkutano wa jukwa la wasanii, kulia ni Mbunifu mkongwe, Asia Idarous na msichana mwenye vipaji vingi, Jokate Mwegelo.
4
Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akifafanua jambo katika mkutano huo.
5
Msanii mkongwe wa maigizo na filamu nchini, Mzee Jangala akifuatilia mkutano wa jukwaa la sanaa.
6
Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akionyesha kipaji chake cha kupiga zeze na kuimba kwa kushirikiana na wasanii wengine waliohudhuria mkutano wa Jukwaa la Sanaa.

Msichana mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo amewataka wasanii kuwa wabunifu ili kupata mafanikio katika sanaa na shughuli zao za kila siku.
Jokate alitoa wito huo wakati akitoa mada katika Jukwaa la Sanaa la lililoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz).
Alisema kuwa sanaa ina wigo mpana sana na kila msanii anatakiwa kuwa mbunifu ili kujiweka tofauti  na msanii mwingine na kujipatia fedha kwa kutumia ubunifu wake.
Kwa mujibu wa Jokate, yeye aliamua kupitia kwenye fani ya urembo na mwaka 2006 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania. Alisema kuwa aliamua kutumia umaarufu wake kujipatia maendeleo pamoja na ukweli kuwa alisomea mambo ya siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Elimu yangu ya mamo ya siasa haina nafasi kwangu, nilianza kuwa mshehereshaji (MC) katika shughuli mbalimbali, nikaingia katika fani ya ubunifu wa mabavi (Kidoti Fashion), nikaanzisha kidoti club ili kupata marafiki ambao tutazungumza lugha moja,” alisema Jokate.
Mrembo huyo hakuishia hapo kwa kuingia katika fani ya utangazaji wa vipndi hasa Chanel O, uigizaji wa filamu, utengenezaji wa nywele, ndala na sasa mwanamuziki.
 “Hii yote ni kutafuta ‘chaneli’ za kupata fedha, nimefanikiwa na sasa nina makubaliano yenye thamani ya Sh 8.5 bilioni na kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti,” alisema.
Mbali ya Jokate, mbunifu maarufu nchini, Asia Idarous naye aliwataka wasanii kuwa waaminifu na kujitangaza katika shughuli zao ili kupata maendeleo.
Idarous  alisema kuwa msanii ambaye atakuwa mbunifu na kipaji cha hali ya juu, hataweza kupata maendeleo kama atakosa sifa ya uaminifu ambayo mara nyingi uendana na nidhamu katika kazi.
“Mimi nilianza kazi ya ubunifu wa mavazi miaka ya 1980, mpaka leo nafanya kazi hii, wabunifu wengi (hata Jokate) amepitia kwangu, siri kubwa ya mafanikio haya ni uaminifu na nidhamu katika kazi, nimefanikiwa kuanzisha Vazi la Khanga nchini Marekani na Lady in Red, leo hii ni maarufu,” alisema Idarous.
Katibu Mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli alitoa wito kwa wasanii chipukizi kufuata nyayo za Jokate na Idarous ili kuweza kufanikiwa katika kazi zao za sanaa.
Bumbuli alisema kuwa ni vigumu kupata mafanikio katika sanaa bila kuweka wazi kipaji chako hadharani na hapo ndipo vyombo vya habari vitakuona na kuanza kuandika habari zao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog