Timu
za taifa ya soka za Afrika Mashariki na Mashariki na Kati ziliaza
michuano ya kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka
AFCON 2017 kwa kupata matokeo mbalimbali.Uganda Cranes wakiwa nyumbani,
katika uwanja wa Kimataifa wa Naambole jijini Kampala walipata ushindi
wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Bostwana.
Vijana wa kocha Milutin Micho walipata mabao yao kupitia nahodha Geofrey Massa na Umony Brian.
Ushindi huo umeendelea kuonesha rekodi ya Uganda kutofungwa nyumbani kwa kipindi kirefu na wamejipatia alama tatu muhimu sawa na Burkina Faso ambao pia waliwafunga Comoros mabao 2 kwa 0.
Mwezi Septemba, Uganda watakuwa ugenini kumenyana na Comoros huku Burkina Faso wakicheza na Bostwana katika kundi hilo.
Tanzania ikiwa mjini Alexandria nchini Misri, walifungwa mabao 3 kwa 0 katika mchuano wao wa kwanza wakiwa ugenini.
Mabao ya Pharaohs yalitiwa kimyani na Rami Rabia, Bassem Morsy huku Mohamed Salha akifunga la tatu na kuihakikishia timu yake ushindi.
Misri sasa itasafiri Chad mwezi Septemba, lakini Tanzania watakuwa nyumbani kuwakaribisha Super Egales ya Nigeria.
Kwa matokeo haya, Misri wana alama tatu sawa na Nigeria ambao waliwafunga Chad mabao 2 kwa 0.
Tanzania na Chad hawana alama yoyote.
Amavubi Stars ya Rwanda ilianza vizuri kwa kupata ushindi ugenini kwa kuifunga Msumbiji bao 1 kwa 0 katika uwanja wa Estadio Nacional Do Zimpeto mjini Maputo.
Bao la ushindi la Rwanda lilitiwa kimyani na Ernest Sugira katika dakika ya tatu ya mchuano huo kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Jacques Tuyisenge. Mambas ya Msumbiji wakiwa nyumbani walitawala mchezo huo na kuishambulia ngome ya Rwanda lakini ikashindwa kupenya katika ngome ya ulinzi.
Kocha Johnny McKinstry sasa inajiandaa kuchuana na Black Stars ya Ghana mwezi Septemba na kwa ushindi wa mwishoni mwa juma lililopita, ina alama tatu sawa na Ghana ambayo iliishinda Mauritus mabao 7 kwa 1.

0 maoni:
Post a Comment