Friday, August 22, 2014


Na Baraka Mpenja
NUSU fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe ka Kagame iliendelea jana mjini Kigali, nchini Rwanda na kupata klabu mbili za kucheza fainali na hatimaye kupatikana bingwa atayechukua kombe lililoachwa na Vital’O ya Burundi.
Katika nusu fainali ya kwanza, El Merreikh ya Sudan ilitinga fainali baada ya kuifunga KCC ya Uganda kwa penalti 3-0.
Mshindi alipatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati kufuatia dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika nusu fainali ya pili, APR walikutana na Wanyarwanda wenzao, timu ya Polisi.
Maafande wa APR walitinga fainali baada ya kushinda kwa penalti 4-3 kufuatia suluhu pacha ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
Katika hatua ya robo fainali iliyomalizika juzi katika uwanja wa Nyamirambo, mechi moja tu ndio ilimalizika ndani ya dakika 90 baina ya KCC ya Uganda na Altabara ya Sudan Kusini.
Mechi ya Azam fc dhidi ya El Merreikh alimalizwa kwa penalti ambapo Wasudan waliibuka na ushindi wa penati 4-3 kufuatia dakika 90 kuhitimishwa kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
Robo fainali nyingine iliwakutanisha Atletico ya Burundi dhidi Polisi ya Rwanda.
Polisi walishinda kwa penalty 9-8 kufuatia suluhu ya bila kufungana katika dakika 90, lakini rekodi iliyowekwa ni wachezaji wote 22 kupiga penalti.
Robo fainali nyingine iliyohitimishwa kwa mikwaju ya penalti ilikuwa baina ya APR na Rayon Sports. Katika dakika za kawaida timu hizi zilitoka sare ya mabao 2-2.
Katika hatua ya nusu fainali mechi zote mbili zilifikia hatua ya mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukomaa ndani ya dakika 120.
Baada ya yote, APR dhidi ya El Merreikh watakutana kesho jumapili katika mchezo wa fainali utakaopigwa uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
Mechi hii inatarajia kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote.

Timu zote zimesheheni vijana wadogo wenye vipaji vya hali ya juu, hivyo kandanda safi linatarajiwa katika dimba hilo la Amahoro ambalo maana yake ni Amani.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog