Friday, August 22, 2014


 LIGI kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 inatarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu kwa timu 14 kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Azam fc. 
Kanuni inasema kuwa ratiba ya ligi inatakiwa kuanikwa hadharani angalau mwezi mmoja kabla ya ligi kuanza, ingawa inaweza kutangazwa hata miezi miwili kabla kama inavyotokea ulaya.
Waendeshaji wa ligi kwa maana ya Bodi ya ligi kuu (TPL Board) na Shirikisho la soka Tanzania, TFF wamekidhi matakwa ya kikanuni baada ya kufanikiwa kuweka hadharani ratiba septemba 20 mwaka huu ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya michuano kuanza. 
Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPL Board) ndio wenye wajibu mkubwa wa kuratibu ligi kuu na ligi daraja la kwanza. 
Uchaguzi wa Bodi ya TPL ulifanyika Oktoba 25 mwaka jana. Oktoba 18 mwaka huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa wakati huo, Hamidu Mbwezeleni alitaja orodha ya mwisho ya wagombea waliokidhi vigezo katika uchaguzi huo. 
Nafasi ya Mwenyekiti alikuwa ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar), Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Waliowania ujumbe wa Bodi ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui). 
Baada ya uchaguzi kufanyika, Mbwezeleni aliwataja washindi ambapo Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar alishinda na kuwa mwenyekiti wa Bodi ya ligi kuu na Said Mohamed wa Azam fc alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti. 
Wagombea hao wawili wa nafasi mbili za juu walitangazwa kupata ushindi wa 100% ya kura zilizopigwa, lakini kwa mujibu wa Mbwezeleni baadhi ya wapiga kura katika uchaguzi huo waliondolewa kwasababu hawakukidhi vikezo.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya uchaguzi aliwatangaza Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui fc).
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamid Mbwezeleni

Kwa mujibu wa Tangazo la uchaguzi wa Bodi ya Ligi lililotolewa Oktoba 14 mwaka 2013 zilitangazwa nafasi tatu kama zinavyoonekana hapo chini pamoja na masharti au sifa zinazotakiwa kuzingatiwa na waombaji:
1.          Nafasi zilizotangazwa kugombewa ni hizi zifuatazo:
(i)          Mwenyekiti  wa  TPL Board.
(ii)        Makamu Mwenyekiti wa TPL Board.
(iii)       Wajumbe wawakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board (TPL Board Management Committee), nafasi mbili (2).
2.          Mtu yeyote  anayeomba nafasi ya uongozi katika TPL Board lazima atimize masharti yafuatayo:
(i)          Awe Raia wa Tanzania
(ii)        Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu elimu ya Sekondari.
(iii)       Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)       Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)         Awe na umri wa angalau miaka 21.
(vi)       Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(vii)     Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TPL Board awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu uliopita (2012/13).
(viii)    Kwa nafasi za  Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu Daraja la Kwanza.

??????????
Mabingwa Azam fc walitoa kiongozi mmoja wa Bodi ya ligi kuu, Makamu mwenyekiti, Said Mohamed

Ukisoma  masharti yaliyotakiwa kuzingatiwa (namba vii) , inasema kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa TPL Board, mgombea alitakiwa awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu wa mwaka juzi (2012/13). 
Kwa nafasi za Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu Daraja la Kwanza.
Hamad Yahya Juma (Mtibwa) na Said Mohamed  (Azam) walikidhi sharti hilo kwasababu msimu wa 2012/2013 timu zao zilikuwa katika nafasi sita za juu.
Kwa upande wa wajumbe, Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui fc), pia walifuzu kigezo hicho kwasababu timu zao zilikuwa ligi daraja la kwanza. 
Lakini katika msimu wa 2013/2014 kulitokea mabadiliko kwa timu zilizotoa viongozi hao.
Azam fc ilitwaa ubingwa kwa upande wa Ligi kuu wakati Mtibwa Sugar ilishika nafasi ya 7 katika Msimamo.
MSIMAMO WA LIGI KUU MWAKA JANA
Standings

Rnk

Team
MP
W
D
L
GF
GA
+/-
Pts


1

26
18
8
0
51
15
36
62


2

26
16
8
2
61
19
42
56


3

26
13
10
3
33
20
13
49


4

26
9
11
6
41
27
14
38


5

26
9
11
6
23
20
3
38


6

26
10
8
8
28
32
-4
38


7

26
7
10
9
30
31
-1
31


8

26
10
1
15
23
40
-17
31


9

26
6
11
9
16
20
-4
29


10

26
6
10
10
26
33
-7
28


11

26
6
8
12
18
35
-17
26


12

26
6
7
13
20
39
-19
25


13

26
3
10
13
19
37
-18
19


14

26
3
7
16
18
39
-21
16

Kwa kuzingatia msimamo huo, viongozi wa nafasi mbili za juu wa Bodi ya ligi kuu kwasasa wanatakiwa kutoka  klabu za Azam fc, Yanga, Mbeya City, Simba, Kagera Sugar na Ruvu Shooting.
Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi

Kwa kuzingatia sharti lilelile, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi kuu, Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar) amekosa sifa kwasababu timu yake msimu uliopita ilitoka nje ya timu sita za juu. Kwa upande wa Said Mohamed ameendelea kuwa na sifa ya kuiongoza bodi hiyo.
Kwa upande wa wajumbe, Pamba fc imeshuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza, kwahiyo Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) kwa mujibu wa masharti yaliyotangazwa amekosa sifa ya kuwa mjumbe.
Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui fc), yeye anaendelea kuwa kiongozi halali kwasababu timu yake ipo ligi daraja la kwanza.
Kwa hiyo Bodi ya ligi kuu ina viongozi wawili ambao hawajakidhi masharti kwasababu ya timu zao kufanya vibaya msimu uliopita.
Tayari msimu mpya unatarajia kuanza septemba 20 na tayari Bodi ya ligi kuu imetangaza ratiba, lakini Mwenyekiti wa Bodi hiyo hatakiwi kuendelea kushika nafasi hiyo kwasababu timu yake haipo kwenye timu sita za juu.
Kwa maana hiyo ilitakiwa kabla ya ligi kuanza, ufanyike uchaguzi mwingine ili kuchagua viongozi wapya, au kama ni ngumu ungefanyika uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi ya mwenyekiti ambaye hana sifa na mjumbe mmoja ambaye amekosa sifa kwa mujibu wa kanuni. 
Kitendo cha kuruhusu ligi ianze bila uchaguzi ina maana wanakiuka taratibu zilizowekwa.
Na kuzingatia masharti yaliyowekwa wakati wa uchuguzi, Bodi ya ligi haina mwenyekiti na inatakiwa uchaguzi ufanyike pamoja na kumpata mjumbe mmoja aliyepoteza sifa kutoka timu ya Pamba.
Hata wale wajumbe walioteuliwa na mwenyekiti wa Bodi kwa ajili ya kuingia kamati ya utendaji ya TFF hawana sifa.
Mwenyekiti wa Bodi anaingia moja kwa moja kwenye kamati ya utendaji kujadili mambo ya mpira, lakini inakuwaje aendelee kupata fursa hiyo wakati hana sifa?
Tatizo linabaki pale pale kuwa viongozi wanaoongoza mpira wa Bongo wana tabia ya kusahau mambo waliyojiwekea wenyewe.
Hamad Yahya alipoteza sifa, muda mfupi baada ya msimu kumalizika ilitakiwa mchakato wa uchaguzi uanze mapema ili apatikane mwenyekiti. 
Lakini ratiba imetoka na ligi inaelelekea kuanza  na kiongozi muhimu wa Bodi hana sifa. 
Ifike wakati tukubali kukaa katika misingi ya kanuni tuliyojiwekea, jambo lipo wazi na ukweli unafahamika, lakini kuna watu wachache wanavunga kama hawaoni hivi. 
Sidhani kama watu wote pale TFF wamesahau, lakini kutokana na mfumo wa kubebana kwa urafiki na masilahi binafsi, watu wasiokuwa na sifa wanaendelea kujadili na kuongoza mpira wa nchi hii. 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog