Mkurugenzi
mtendaji wa Airtel Bwana Sunil Colasa akiongea na waandishi wa habari
leo hii (hawapo pichani) akiwatangazia kuanza kutumika rasmi kwa huduma
mpya ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa
moja kwenye akaunti zao za Airtel money, (interoperability) huduma hii
ni ya kwanza Duniani ambapo inaaminika kuwa itasaidia sana wateja wa
Airtel Money na Wakala kuokoa muda wa kupata na kutoa huduma kwa haraka
Zaidi.
=========== ==========
- Wateja Airtel Money sasa wanaweza kutuma na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money toka Tigo Pesa
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma itakayowawezesha wateja
wake wa huduma ya Airtel Money kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye
mitandao mingine moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel money ,
huduma hii ni ya kwanza Afrika na duniani kwa ujumla na hivyo inaweka
historia nchini kuzinduliwa ya kwanza kupitia njia ya mtandao wa simu.
Huduma
hii ya kwanza Duniani na Afrika inayohusisha makampuni ya simu Airtel
na Tigo ulitangazwa kuwa itaanza kutumika mwishoni mwa mwezi wa Julai na
sasa iko tayari ambapo wateja wa Airtel Money wataweza kutumia huduma
hii kabambe na yenye utofauti kwa inaaminika kuwa ni rahisi zaidi,
salama na ina unafuu katika kutuma pesa kwa kutoka mteja mmoja kwenda
mwingine na kuingia moja kwa moja katika (e-wallet) akaunti yake ya
simu/mtandao anaotumia na kuweza kuitoa popote alipo.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Airtel Bwana Sunil
Colaso alisema” Tunayofuraha kushirikiana na makampuni mengine ya simu
katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma za kisasa, zenye ubunifu na
kwa gharama nafuu. Ushirikiano huu utawawezesha wateja wa Airtel kutuma
na kutoa pesa kutoka kwenye mitandao mingine .
Sasa
wateja wetu watapokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine na kuingia
moja kwa moja kwenye (e-wallet) akaunti zao za Airtel money hivyo
kuondoa usumbufu ulikuwepo awali ambapo mteja anapotumiwa pesa kutoka
mtandao mwingine alitakiwa kuzitoa ndani ya siku 7.
Kwa uzinduzi huu leo tunafanya huduma hii ya kifedha kwa njia ya mtandao kukidhi mahitaji ya wateja. Vile
vile mawakala wetu pia wamerahisishiwa utoaji huduma ambapo sasa
hakutakuwa na haja ya wakala kupata udhibitisho wa ujumbe kutoka kwa
simu ya mteja kabla ya kufanya malipo. Tunaamini huduma hii itaongeza
usalama wa mawakala na wateja nchini, Pia itamuongezea wakala muda wa
kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa uhakika, haya ni mapinduzi ya huduma za
kifedha ambayo tunaamini ni maendelea makubwa ya maboresho ya huduma
hii aliongeza kwa kusema Colaso.
Akiongea
kuhusu huduma hiyo mmoja wa wakala ambae alijaribu wa Airtel Money
Pasco Woiso alisema “Tunafurahia huduma iliyoanzishwa na Airtel kwa
kushirikiana na mitandao mingine, leo nimeitumia huduma hii kwa mara
ya kwanza lakini nimefurahishwa na ufanisi wake na jinsi wateja
wanavyoipokea vizuri nikiwapasha habari kuhusu huduma hiii.
Kwa
sisi wakala awali tulikuwa na tatizo la kupata ujumbe wa malipo,
kitambulisho cha malipo na pesa kurudi baada ya muda wa siku saba,
lakini kwa sasa ushirikiano huu umeifanya huduma hii ya pesa kwa
mtandao kuwa bora zaidi na kupunguza muda niliokuwa nautumia kumuhudumia
mteja moja na hivyo.
0 maoni:
Post a Comment