‘Mimi na Yanga tulikua na makubaliano ya mkataba na hakuna
ukweli kwamba Mshahara niliokua nalipwa Yanga ni mdogo, mshahara usingekua
unatosha nisingekubali kusaini mkataba‘
‘Ni kweli kuna
mambo mengi hayapo sawa kati yangu na club yangu yaYanga ila ni mambo ya ndani ambayo nisingependa
kuyazungumzia, ni mambo madogo ambayo nadhani yanaweza kuisha‘
‘Hakuna ukweli kwamba mimi nakwenda Ulaya, sijui
hata imetoka wapi na nani kaanzisha hii ya Ulaya, mimi bado ni mchezaji halali
wa Yanga na huwa naongea nao karibu kila siku, hata jana nimetoka kuongea na
katibu mkuu na mambo yote yanaelekea vizuri hamna shida yoyote mpaka sasa hivi‘
- Hii ni kauli ya mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Anord Okwi.
0 maoni:
Post a Comment