MABINGWA
wa Bundesliga Bayern Munich wataanza kampeni za kutwaa Taji la Ubingwa
wa Germany kwa mara ya 25 wakiwa Nyumbani Allianz Arena Ijumaa Usiku kwa
kucheza na Wolfsburg.
Msimu uliopita, wakiwa chini ya Meneja Pep Guardiola, waliweka Rekodi ya kutwaa Ubingwa mapema mno waliposhinda Taji hapo Machi 25 ikiwa karibu Miezi miwili kabla Msimu kumalizika.
Wolfsburg walimaliza Msimu uliopita wakiwa Nafasi ya 5.
Lakini tayari Msimu huu Bayern wameshajeruhiwa baada ya Wiki iliyopita kuchapwa Bao 2-0 katika Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea DFL Supercup huko Signal Iduna Park walipocheza na Mahasimu wao Borussia Dortmund.
Moja ya Mechi kali za Wikiendi ya Ufunguzi wa Msimu wa 2014/15 ni hapo Jumamosi Agosti 23 kwenye mtanange utakaochezwa Signal Iduna Park wakati Borussia Dortmund watakapokuwa Wenyeji wa Bayer Leverkusen.
Dortmund, chini ya Kocha Jurgen Klopp, walimaliza Ligi wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 19 nyuma ya Bayern Munich na wataivaa Bayer Leverkusen ambayo itakuwa chini ya Meneja mpya Roger Schmidt.
BUNDESLIGA
RATIBA
Mechi za Ufunguzi
Ijumaa Agosti 22
21:30 Bayern Munich vs VfL Wolfsburg
Jumamosi Agosti 23
16:30 Hannover 96 vs Schalke 04
16:30 Hertha Berlin vs SV Werder Bremen
16:30 Eintracht Frankfurt vs SC Freiburg
16:30 FC Köln vs Hamburger SV
16:30 TSG Hoffenheim vs FC Augsburg
19:30 BV Borussia Dortmund v Bayer 04 Leverkusen
Jumapili Agosti 24
16:30 SC Paderborn 07 vs FSV Mainz 05
18:30 Borussia Mönchengladbach vs VfB Stuttgart

0 maoni:
Post a Comment