Walizinguana: Argentina Sergio Aguero na Marcos Rojo walitamkiana maneno makali katika fainali za kombe la dunia.
MECHI
ya watani wa jadi nchini England baina ya Manchester United na
Manchester City “The Manchester derby” itakuwa na ladha tofauti msimu
huu ambapo nyota wawili wanaocheza timu ya taifa ya Argentina, Sergio
Aguero na Marcos Rojo watakutana.
Wachezaji
hao wawili waliocheza fainali ya kombe la dunia walisemekana kutamkiana
maneno makali wakati wa mashindano ya majira ya kiangazi nchini Brazil
baada ya Rojo ambaye amekamilisha kujiunga na Manchester United kwa
paundi milioni 16 kutoka klabu ya Sporting Lisbon kumkaribisha rafiki
yake, mkali wa muziki wa Pop nchini Argentina, El Polaco ndani ya
chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo wa makundi.
0 maoni:
Post a Comment