Kijana mpya: Leroy Fer akionesha jezi yake namba 10 atakayovaa QPR .
KIUNGO wa Kiholanzi, Leroy Fer amekamilisha usajili wake wa kujiunga na QPR akitokea klabu inayocheza Championship, Norwich.
Nyota huyo mwenye miaka 24 ambaye
amesajiliwa kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7, amesaini mkataba wa
miaka mitatu na kikosi cha kocha Harry Redknapp.
Fer amecheza kwa msimu mmoja katika dimba la Carrow Road baada ya kujiunga na timu hiyo kutokea timu ya Eredivisie ya FC Twente msimu uliopita.
Nyota kinda: Fer akisaini mkataba wake, pembeni yake ni mke wake Xenia Schipaanboord
0 maoni:
Post a Comment