Manchester United wamemsaini Marcos Rojo kutoka Klabu ya Sporting Lisbon.
Manchester United imetangaza rasmi kumsaini Beki wa Sporting Lisbon Marcos Rojo kwa Ada ya Euro Milioni 20 na kumpa Mkataba wa Miaka Mitano.
Kwenye Dili hiyo, Nani amekwenda Sporting Lisbon kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
Rojo, mwenye Miaka 24, alihamia Sporting Lisbon Mwaka 2012 akitokea Spartak Moscow.
Rojo atavaa jezi No.5 na amesaini tayari miaka mitano na Klabu hiyo ya Mashetani Wekundu
Beki huyo alicheza Mechi zote za Argentina huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia, na kufunga Bao 1 dhidi ya Nigeria, na Argentina kufika Fainali iliyofungwa Bao 1-0 na Germany.
Umahiri wake ulimfanya awemo kwenye Timu ya FIFA ya Fainali za Kombe la Dunia za Brazil 2014.
Kabla kuhamia Spartak Moscow na kisha Sporting Lisbon, Rojo aliichezea Estudiantes ya Argentina na kutwaa Copa Libertadores Mwaka 2009.
Mara baada ya kukamilisha Uhamisho huu, Rojo alisema: “Ni heshima kubwa sasa kutamka naichezea Manchester United. Ligi Kuu England ni Ligi kubwa Duniani na kupata nafasi kuichezea Klabu kubwa kabisa Duniani ni ndoto kwangu. Mimi bado Kijana na nina ari kuendelea kujifunza na kucheza chini ya Kocha mzoefu Louis van Gaal!”
Nae Meneja Louis van Gaal amesema: “Marcos ni Beki mwenye kipaji. Amecheza Soka la kiwango cha juu kabisa na anaweza kucheza kama Sentahafu au Fulbeki wa Kushoto. Ana uwezo, nguvu na nia ya kujifunza na hii inamaanisha mwisho wake ni mzuri. Alicheza vizuri kwenye Kombe la Dunia na amecheza Ulaya kwa Miaka kadhaa sasa. Ni nyongeza nzuri kwa Timu!”
Marcos Rojo aliwasili jana usiku England tayarikwa kukipiga na Manchester United
Rojo akiwasili
Rojo tayari aliwasili kwenye Hospitali ya Bridgewater kwa Vipimo
0 maoni:
Post a Comment