Mimi sipo!: Tim Sherwood jana ametangaza kuwa hatakuwa kocha Crystal Palace .
TIM Sherwood amejitoa mwenyewe katika mbio za kuwa kocha mpya wa Crystal Palace.
Kocha huyo wa zamani wa Tottenham
Hotspur alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa
Selhurst Park baada ya Malky Mackay kuondolewa katika kinyang'anyiro.
Lakini Sherwood hajavutiwa kurithi
mikoba ya kocha aliyeondoka Tony Pulis, na hii inamaanisha Keith Millen
ataendelea kuiongoza timu hiyo kwa muda katika mechi ijayo ya ligi kuu
dhidi ya West Ham uwanja wa nyumbani.
Siendi: Sherwood anasema hajavutiwa na kazi hiyo na amethibitisha kuwa hatarithi mikoba.
"Palace ni klabu kubwa yenye utamaduni
wake, lakini ipo katika hali ngumu ambayo haiwezi kuonekana kirahisi,"
Sherwood aliwaambia Sky Sports.
Makubaliano binafsi baina ya Sherwood na
Palace yalishindwa kufikia muafaka baada ya kuripotiwa kuwa kocha huyo
alitaka kuwa pamoja na wasaidizi wake wakati akiwa Spurs, Chris Ramsey na Les Ferdinand katika dimba la Selhurst Park.
Mmiliki wa Palace, Steve Parish aligoma
mapendekezo hayo na sasa anaangalia uwezekanao wa kupata kocha mpya
zikisalia saa 48 tu klabu hiyo ijitupe uwanjani katika mchezo wa ligi
kuu.
0 maoni:
Post a Comment