Thursday, August 21, 2014


Wanted: Roma have asked about the availability of Chelsea striker Fernando Torres
Anawindwa: Roma wanaitaka saini ya Fernando Torres 

ROMA wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Cheslea, Fernando Torres.
Timu hiyo ya Italia, inaitaka saini ya mshambuliaji huyo wa Hispania, na watawashawishi The Blues kumchukua Mattia Destro kama sehemu ya dili hilo.
Torres amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge Stamford Bridge kutokea Liverpool kwa ada kubwa ya uhamisho ya paundi milioni 50 mwezi januari 2011.
Kocha Jose Mourinho ameongeza wachezaji katika safu ya ushambuliaji majira haya ya kiangazi ambapo amemsajili Diego Costa kwa paundi milioni 32 na kumrudisha gwiji wa Chelsea, Didier Drogba.
Tayari Roma walishamsajili nyota mwingine wa zamani wa Cheslea, beki wa kushoto, Ashley Cole kama mchezaji huru.
Part of the deal: Roma are seeing whether Chelsea would be keen to take Italian frontman Mattia Destro
Sehemu ya dili: Roma wanataka kuwapatia Mattia Destro kama sehemu ya usajili wa Torres.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog