Dakika ya 65 kipindi cha pili Jesse Lingard anapatia bao la pili Man United kwa msaada ya Tyler Blackett, Sasa ni 2-0.
Kipindi cha pili dakika ya 63 Kikosi cha man United kilibadilishwa karibu chote na kuingia wengine. Mwamuzi wa mechi hii alikuwa ni Baldomero ToledoMchezaji wa Zamani wa Liverpool Louis Suarez akiachia shuti kali lililomzidi Daley blind Wayne Rooney na Gerard Pigue wakikabana Ashley Young na Adriano wakiruka juu kuutafuta mpiraWayne Rooney dakika ya 8 anaifungia bao la kuongoza Man United akipata usaidi kutoka kwa Ashley Young.
Mbele ya Mashabiki 68,414 ndani ya Levi's Stadium huko Santa Clara, Californina, Manchester United imewafunga Mabingwa wa Ulaya na Spain Barcelona 3-1 kwenye Mechi ya Kitafiki ambayo ni mfululizo wa kugombea International Champions Cup.
Wayne Rooney akishangilia bao lake la mapema dakika ya 8.
Kepteni wa Man United Wayne Rooney ndie aliefunga Bao la kwanza alipounganisha kwa Kichwa Kona ya Ashley Young.
Mara tu baada ya Meneja Louis van Gaal kubadili Kikosi chake kizima baada ya Dakika 60, Man United walifunga Bao la Pili kupitia Jesse Lingard baada kuunganisha Krosi ya Tyler Blackett.
Wachezaji hao 11 walioingizwa ni Johnstone, Valencia, Smalling, McNair, Blackett, Lingard, Fellaini, Herrera, Wilson, Pereira na Januzaj. Suarez aligonga mwamba hapa
Katika Dakika ya mwisho, Rafinha aliipa Barca Bao lao pekee lakini hapo hapo Adnan Januzaj akaipigia Man United Bao lao la 3.
Huu ni ushindi wa 3 katika Mechi zao zote 3 kwa Man United huko Ziarani USA walipoanza kwa kuifunga Club America ya Mexico na kufuatia ushindi dhidi ya Klabu ya Marekani San Jose Eartquakes.
Man United watacheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Paris Saint-Germain hapo Jumatano.Suarez akiwekwa chini na Darmian
0 maoni:
Post a Comment