Monday, July 27, 2015

IMG_5796
Baraka Kizuguto msemaji wa TFF
Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA limetangaza mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mechi za robo fainali ya michuano hiyo.. CECAFA imetangaza mabadiliko hayo kupitia kwa msemaji wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto.
cecafa
Mabadiliko yaliotangazwa hapo ni ya mechi za robo fainali, mchezo wa kwanza utapigwa saa 7:45 ambapo itakuwa mechi kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Khartoum ya Sudan na mchezo wa pili utapigwa saa 9:45 utakutanisha timu ya  Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini, michezo hiyo itapigwa July 28.
KMKM-vs-Gor-Mahia-1
Kikosi cha Gor Mahia ya Kenya
July 29 itapigwa michezo miwili wa kwanza utakuwa mchezo kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya AL Shandy ya Sudan saa 7:45 na mchezo wa pili ni kati Azam FC  dhidi ya Yanga saa 9:45 michezo yote itapigwa katika Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na hakutakuwa na dakika 30 za nyongeza kama timu zitatoka suluhu bali zitapigiana mikwaju ya penati.
NUTTALL-THINK
Kocha wa Gor Mahia Frank Nutall
Sambamba na mabadiliko hayo CECAFA pia imewaandikia barua ya kuwapa onyo klabu ya Gor Mahia ya Kenya na kocha wao Frank Nutall kwa utovu wa nidhamu kwa kutumia mlango ambao hawakupaswa kutumia wakati wa kuingia na kutoka vyumbani.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog