Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye
pia amewahi kuitumikia klabu ya Chelsea ya Uingereza kwa miaka kadhaa
sasa ameamua kuendeleza maisha yake ya soka Canada na ataanza kuonekana
katika Ligi Kuu ya Marekani MLS.
Taarifa zimethibitisha kuwa Drogba amekubaliana na klabu Montreal Impact na atajiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi 18, Drogba amekuwa akiwindwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Marekani toka mwaka 2012 na alikataa mshahara wa dola milioni 7.5 kwa mwaka na kutimkia China.
Rais wa klabu ya Montreal Impact Joey Saputo amethibitisha Drogba kujiunga na kikosi chao.
“Ni
heshima kumkaribisha Drogba katika klabu ya Montreal Impact, toka
mazungumzo yetu ya kwanza nazungumza nae, nilijisikia kwamba kiukweli
alitaka kuichezea Montreal”>>>Joey Saputo
0 maoni:
Post a Comment