Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anajulikana kwa majigambo, kujisifia lakini pia anapenda kitu kizuri kiwe kwake.
Kama utakua unakumbuka vizuri Mourinho
ni kocha anayependa mfumo wa kujihami kwa lugha za mpira wanaita kupaki
Bus yaani ni mfumo ambao timu inashambulia kwa kushtukiza na kujihami
kwa kiasi kikubwa… Lakini cha kushangaza aliwahi kukutana na timu yenye
tabia zaidi ya zake alilalamika.
Sasa basi Mourinho
amerudi tena kwenye headlines, kwa kuanza kejeli zake tena kwa kusema
kuwa timu pinzani zina jaribu kununua mataji. Mourinho ameyasema hayo
kufuatia klabu vya Manchester United kufanya usajili mkubwa msimu huu, kwa wachezaji kama Matteo Darmian, Memphis Depay, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin vivo hivyo kwa upande wa Man City na Klabu ya Liverpool ambao nao wamefanya usajili kwa kutumia fedha nyingi.
Licha ya kukiri kuwa hata mwaka 2003 mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich alikuwa ananunua mataji klabuni hapo baada ya kuanza kununua wachezaji kwa gharama ya juu, kauli ya Mourinho inatafsirika
kama hapendezwi na usajili wanaofanya timu pinzani licha ya kuwa soka
limebadilika wamiliki wananunua wachezaji kwa gharama za juu.
0 maoni:
Post a Comment