2015 tumeshuhudia mastaa mbalimbali wa kike na wa kiume Tanzania wakitangaza nia ya kuingia bungeni akiwemo mwimbaji wa Taarab Mzee Yusuf, Profesa Jay, Steve Nyerere na kwa Wanawake waliojitokeza kuziwania nafasi za Ubunge wa viti maalum ni pamoja na waigizaji Wema Sepetu na Wastara, na msanii wa bongofleva Ksher.
Wema Sepetu na Wastara hawakupita kutokana na kukosa kura za kutosha lakini Khadija Shaaban (Ksher) amepita tena ambapo alithibitisha hayo na wakati mwingi kwenye maneno yake ya kujinadi ni ‘mara nyingi watu wanakosa uthubutu kutokana na kutojiamini kuwa vile walivyo wanaweza kufanya mambo makubwa ya ajabu bila kujali kiwango cha elimu, pesa au mtandao alionao’
Kwa upande wa Wastara, kwenye kura za maoni zilizopigwa akiwania Ubunge wa viti maalum kupitia Walemavu, zilipigwa kura 759, zikaharibika 40 huku Magreth Mkanga akipata kura 424, Wastara akishika nafasi ya pili kwa kuchukua kura 254 na Chausiku Lukinga 43.
0 maoni:
Post a Comment