Thursday, June 30, 2016

Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini. Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)...
Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Petro Marwa kwenye  maonesho ya  kimataifa ya  sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar...
Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo. Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao...
Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,...
KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda. Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni...
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na mke wa tajiri namba moja duniani na mwenyekiti mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Melinda Gates kwa pamoja wamelipongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kwa kufanya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kama moja ya mbinu za kumkomboa mwanamke mnyonge kiuchumi. Wawili hao waliyasema hayo kwenye mdahalo uliofanyika...
...
Wateja wakipata maelezo kuhusu huduma za TTCL, katika viwanja vya sabasaba  Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.  TTCL wakitoa huduma kwa wateja katika maonesho ya Sabasaba   Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.  Wafanyakazi wa TTCL wakiwakaribisha wateja katika Banda. Wananchi ...
 Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016. Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la...
Meneja wa kituo cha kusimamia wasanii ‘Mkubwa na Wanae’ Said Fella ameelezea ndani ya miaka mitano kituo chake kimefanya kitu gani kwenye tasnia ya Bongo Fleva na mabadiliko yaliyoonekana. ‘Mpaka sasa hivi Mkubwa na wanae ina miaka mitano na kuna vitu vingi vilivyofanyika na watu wanaona,...
Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo June 30 imetangaza rasmi kupitia kurasa zake za mitrandao ya kijamii kuingia mkataba na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog, Simba wametangaza kuingia mkataba na Omog bila kuweka wazi mambo kadhaa kwa kigezo kuwa taarifa rasmi itatoka kesho July 1. Simba wameingia mkataba na Omog ambaye amewahi kuifundisha...
Burudani Rapper kutoka Bongoflevani, Darasa anayetamba na wimbo uitwao Kama  Utanipenda aliyomshirikisha Rich Mavoko , sasa leo June 30, 2016 alikutana na waandishi wa habari kwaajili ya kuzinduzi single yake mpya iitwayo Too Much. Wimbo huo mpya umeandaliwa kwenye kipindi cha miezi sita iliyopita kupitia studio ya Mr....
ENGLAND inatafakari uwezekano wa kumteua Gareth Southgate awe Meneja wa Muda wa England kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson mara baada ya England kutupwa nje ya EURO 2016 kwenye Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Iceland huko France. Southgate, ambae sasa ndie Bosi wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 21, U-21, anaweza kuteuliwa ili kuisimamia Timu hiyo...

Wednesday, June 29, 2016

Mkali wa Bongo fleva, Harmonize ambaye ni msanii wa kwanza kusainiwa kwenye lebo ya Diamond Platnumz (WCB), amekaa kwenye interview hii na Millard Ayo na amezungumzia kuhusu kujiendeleza zaidi katika masuala ya lugha, Harmonize amesema… >>>’Kuna mwalimu pale ofisini...
Liverpool wamekamilisha kumsaini Sadio Mane kwa Dau la Pauni Milioni 34 kutoka Southampton na kumpa Mkataba wa Miaka Mitano. Dau hilo linaweza kupanda na kufikia Pauni Milioni 36 likizidi lile la Mchezaji alienunuliwa na Liverpool kwa ghali kupita yeyote walipotoa Pauni Milioni 35 kumnunua Andy Carroll Mwaka 2011. Dili hii imemfanya Mane, anaetoka Senegal, kuwa ndie Mchezaji wa Bei...
Leo June 29 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole ‘CHADEMA’  jimbo la Longido kutokana na udanganyifu. Akisikiliza kesi hiyo Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c za ubunge...
June 28 2016 ziliripotiwa taarifa kuwa watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania. Leo June 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe...
Imeripotiwa kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza...

waliotembelea blog