Mbunge
wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano
vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo
kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na
kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi
wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao
kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika
kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya
kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa
kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia
adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.
0 maoni:
Post a Comment