Wateja wakipata maelezo kuhusu huduma za TTCL, katika viwanja vya sabasaba
Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.
TTCL wakitoa huduma kwa wateja katika maonesho ya Sabasaba
Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.
Wafanyakazi wa TTCL wakiwakaribisha wateja katika Banda.
Wananchi
waendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Kampuni ya Simu
Tanzania(TTCL) kununua bidhaa bora za 4G katika viwanja vya Maonesho ya
Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba.
Akizungumza
katika Maonesho hayo, Emerco Mashele Afisa kutoka TTCL amesema kuwa
katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya SabaSaba, kampuni
imeendelea kuwaletea watanzania bidhaa nzuri za 4G – LTE, zenye kiwango
kikubwa cha ubora, bei nafuu na uhakika.
“Safari
hii tumewaletea Wananchi bidhaa bora na nzuri katika matumizi ya
mawasiliano ya simu. Kwa huduma zetu tunatoa fursa kwa wateja wetu
kupata intaneti yenye kasi ya 4G ukiwa na Laini za 4G ambazo
zinapatikana hapa katika Banda TTCL na ofisi za TTCL katika jiji la Dar
es salaam” amesema Emerco.
Aidha,
Bw. Emerco aliongeza kuwa katika Maonesho haya ya SabaSaba, TTCL inatoa
fursa ya wananchi kupata laini ya 4G, Modemu ya 4G, Mi-Fi ya 4G na
Routers ya 4G.
Katika
maonesho haya tuna laini za 4G ambazo zinapatika hapa na katika ofisi
zetu za TTCL, Mteja anaweza kifaa cha 4G Mi-Fi ambapo mteja anaweza
kuunganisha watu wengine 10 na kupata intaneti katika ubora ule ule. 4G
Routers inauwezo wa kuunganisha watu 32 na inauwezo kwenda katika ubora
ule ule, Aidha pia Routers inatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma simu
ya Mezani.
0 maoni:
Post a Comment