Tundu
Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo
kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.
Upande
wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola
akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum
Mohammed.
Kongola
alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam
mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na kudharaurisha watanzania dhidi ya
mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alinukuu
maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara
inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta
uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa
kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene"
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.
upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande
wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo,
Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni
mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.
alitimiza masharti atasomewa maelezo ya awali Agosti 2,2016.
0 maoni:
Post a Comment