KONGAMANO
kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki
walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la
utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa
makampuni na viwanda.
Kongamano
hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya
viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa
makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na
Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na
namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa
kati unaotegemea viwanda.
Wengine
waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo
yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki
ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia
ufumbuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika
ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa
nchini, Mh. Malika Berak.(Picha na Modewjiblog)
Taasisi
ya utoaji mafunzo ya Ufaransa ya AFPA ndiyo ilikuwa inaendesha mafunzo
hayo wakibadilishana uzoefu na wadau wa Tanzania kutoka sekta binafsi.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kida alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi katika
kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto zinazojitokeza na fursa zilizopo
katika mafunzo, ukuzaji na uendelezaji taaluma.
Dkt.
Kida alifurahishwa na mchanganyiko wa watu kutoka sekta binafsi
waliofika katika kongamano hilo ambao aliamini kwamba wataelezea uzoefu
wao katika kukabiliana na changamoto za taaluma katika makampuni yao.
Aidha
alisema kwamba wadau hao wa Tanzania watapata uzoefu wa timu ya
wataalamu wanne kutoka kwa wakala wa mafunzo ya taaluma nchini Ufaransa
(AFPA) ambao wataeleza miaka 60 ya uzoefu katika masuala ya mafunzo ya
taaluma na uendelezaji wa utaalamu.
Balozi
wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kushoto) akibadilishana mawazo na
mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald
Mengi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida katika ofisi za ESRF jijini
Dar es Salaam.
Alisema
anaamini kwamba mchanganyiko huo wa wadau utasaidia katika kukabiliana
na tatizo la taaluma katika soko la ajira la Tanzania.
Alisema
mazungumzo hayo ni muhimu sana katika kuibua fursa hasa wakati taifa
hili linajipanga kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda na bila
wataalamu wenye taaluma zao makamapuni na viwanda vingi vitakuwa na
shida kubwa.
Alisema
changamoto kubwa inayokabili taifa la Tanzania kuelekea nchi ya viwanda
kama ilivyo katika nchi nyingine zinazoendelea ni ukosefu wa taaluma na
utaalamu.
“Ukosefu
wa wafanyakazi wenye taaluma katika ngazi zote ni tatizo kubwa
linalokabili harakati za kuelekea uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Kida.
Anasema
pamoja na matatizo hayo taasisi yake tayari imeshaanza kushughulikia
shida hiyo ya taaluma nchini Tanzania kwa kuwa na makongamano mbalimbali
makubwa yanayokutanisha wadau kuzungumzia hali hiyo.
0 maoni:
Post a Comment