Leo June
29 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi
yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ jimbo la Longido kutokana na
udanganyifu.
Akisikiliza
kesi hiyo Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika
matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c za ubunge
hivyo uchaguzi utarudiwa.
Kesi hiyo ilifunguliwa mnamo June 29
2016 mahakama kuu Arusha na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi ‘CCM’ jimbo la Longido Dk. Steven Kiruswa.
Baada ya ushindi wa kesi hiyo dhidi ya Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ Dk. Kiruswa ‘CCM’ amesema…..>>>’tunangojea
wenzetu kama wana sababu ya kukata rufaa, wakate baada ya hapo tutaenda
uwanjani kuanza upya….tulikuwa na madai mengi ya msingi lakini moja ni
kuwepo kwa kasoro katika utaratibu waliotumia kuhesabu, kujumlisha na
kutangaza matokeo ya uchaguzi‘
0 maoni:
Post a Comment