Imeripotiwa
kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki na wengine
zaidi ya 100 kujeruhiwa, shughuli za usafirishaji katika uwanja huo
zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea.
Gavana wa
mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu haona idadi hiyo ya
majeruhi. Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu ambapo mmoja
kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa
kujilipua kwa bomu na kufa.
Hata hivyo
mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja
huo. Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na
kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
0 maoni:
Post a Comment