Na Amplifaya Amplifaya
Unapata maana ya kwamba Pele anatambua kile au ni kipi unataka kumuuliza hata kabla haujaanza kubuni maneno.
Labda ni kitu asili
chenye muingiliano na uelewa sawa wenye athari kwa tabia za binadamu na
jinsi gani anaweza kutumia hiyo fursa kwa faida yake ambayo imemfanya
kuweza mchezaji mkubwa na mwenye historia kubwa duniani pia mwenye
rekodi ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi duniani ambapo katika mchezo
wa soka haijawahi kutokea.
Au labda kiurahisi ni kama sababu ya marejeo au kitu kisichoweza kuepukika kimazoezi.
Mchezaji huyo ambaye ni
mshindi mara tatu wa kombe la dunia akiwa na timu yake ya Taifa ya
Brazil labda hakumbuki amefanya mahojiano mara ngapi na vyombo vya
habari na jinsi alivyotambulika katika umma wa watu duniani, magoli yake
ambayo yanahesabika kuwa ni 1284 katika michezo yake yote aliyocheza na
ikiwa kama amepata stashahada ya rekodi ya dunia.
Pele atakuwa anafikisha
miaka 75 mwaka huu (amezeeka sasa) lakini haoneshi dalili yotote ya
kupumzika na kuachana na masuala ya soka maana amekuwa akijumuishwa
katika masuala mengi ikiwemo matangazo, projekiti nyingi kuhusiana na
soka kiujumla huku akizunguka takribani dunia nzima.
Hauhitaji kujitambulisha mwenyewe na kila mtu anajua Pele ni nani.
Mwishoni mwa wiki
iliyopita moja kati ya majukumu yaliyompeleka Pele Uingereza alikuwa ni
mmoja kati ya wageni maalum pale Anfield ambapo Liverpool iliwakaribisha
Manchester United na mchezo kumalizika kwa Liverpool kufungwa mechi
hiyo katika ligi kuu ya Uingereza.
“Ni furaha kuwa hapa” Pele alisema wakati akiongea na mwandishi mmoja wa habari”
“Kuja Uingereza zaidi ya mara moja ni kitu cha kujivunia zaidi” Pele alisema.
Brazil huwa tuna kila
mechi kila ifikapo mwisho mwa wiki kupitia video na Uingereza pia ambayo
ni ligi moja muhimu sana hapa Duniani. Alisema
Kunaweza kuwa na baadhi
ya wachezaji wengi wa Kibrazil ambao wanatumikia maisha yao ya soka na
vilabu ya Uingereza lakini nyota wakubwa watabakia kuwa nyota wa
kipekee, na hapo ndipo mazungumzo yalipogeukia kwa Neymar ambaye ndiyo
anaaminiwa na Pele kuwa ni nyota wa Barcelona hasa kwa hizi siku zijazo
za usoni akiwa na maana ya miaka ijayo mbele.
“Hakuna jipya, nineongea sana kuhusu Neymar” Pele alisema
“Ni kama mtoto wetu tu,
alichezea Santos, nilichezea Santos na mwanangu Edinho alichezea Santos
kama golikipa na hivyo tunafurahia kuwa na Neymar
Nadhani kiwango chake
tokea mwaka jana hadi sasa kimeimarika zaidi na bado ana mambo mengi
zaidi ya kujifunza akiwa kama mchezaji japo ni mchezaji mzuri” Pele
alisema.
Kumbuka kuwa Pele
alishawahi kuwa mmoja wa watu waliopinga sana Neymar asiondoke Barcelona
ili kulinda kiwango chake ndani ya Kilabu cha Santos na sio Barcelona
tu halikadhalika Real Madrid na vilabu vingine.
Itakuwa ni kitu cha
kujivunia zaidi kucheza Barcelona sababu Barcelona sio timu tu bali ni
Messi na Neymar, Pele alisema kuwa Messi ni mchezaji bora ambaye
hajawahi kumuona katika maisha yake ya soka na anasema licha ya kuwa
Barcelona bado kuna wachezaji wengine ambao ni nguzo ya timu kama Xavi
na Iniesta jinsi wanavyocheza wana mchango mkubwa sana katika timu.
Pele pia alizungumzia
suala la FIFA kubadili ratiba ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 ambapo
litakuwa linachezwa majira ya masika mwezi wa 12.
” nadhani wiki hii
ndiyo wameamua kombe lichezwe mwezi wa 12 kipindi ambacho kitakuwa ni
cha majira ya joto kwetu Brazil, kitu kizuri ni kuliweka kombe katika
mazingira mazuri kwa watu, mahali na wakati sio jambo muhimu bali ni
kitu ambacho kinachanganya mno, mabadilikobya kucheza mwezibwa 12 sio
madogo kabisa” Pele alisema.
0 maoni:
Post a Comment