Baraza
la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium
Lager wamezindua rasmi msimu mwingine wa tuzo za muziki Tanzania
unaojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli amesema; “Kilimanjaro
Premium Lager ni bia ya watanzania na imejikita katika kuwaletea
burudani na pia kutoa majukwaa ambayo yanawapa Watanzania fursa ya
kukuza vipaji mbalimbali.. hii tumeithibitisha kwa juhudi za makusudi za
kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalaam mbali mbali
kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani
tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu kuongezeka kwenye medani
za Kimataifa.”
Kampuni hiyo imewekeza zaidi ya Tshs. Bil.1 kuhakikisha ubora wa hali ya juu unajitokeza kwenye mchakato mzima wa tuzo hizi.
Msimu huu hauna mabadiliko makubwa sana katika vipengele wala mfumo wa
kuwapata wasanii watakaoshiriki, kuna maboresha kwenye njia za upigaji
kura kwa mfano kwa sasa ni watu wengi wanatumia Whatsapp, KTMA
imewarahisishia kwa kuongeza njia hiyo kwenye mchakato wa kupendekeza na
kupiga kura.
Kura za maoni zitaanza kupigwa tarehe March 30 ambapo shabiki ataweza
kupendekeza nani ama nyimbo zipi ziwemo kwenye vipengele vyote vya KTMA
2015.
Watu watapiga kura kupitia mtandao, Whatsapp na SMS na utaratibu uliopo
ni kwamba namba moja ya simu itatumika kupiga kura moja kwenye kila
kipengele.
0 maoni:
Post a Comment