Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu
akiuguza majeraha, hatimaye kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid
James Rodriguez arejea mazoezini kufuatia matibabu mazuri aliyopatiwa
na madaktari wa timu hiyo.
Rodriguez,23, alivunjika mfupa wa ndani katika mguu wake wa kulia mapema mwezi Februari katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa na
matajiri hao msimu huu kwa ada ya paundi milioni 63 kutoka Monaco mpaka
anapata majeraha hayo tayari alishaifungia klabu hiyo magoli 7 na kutoa
pasi za mwisho 7 katika mechi 22 alizocheza kwenye michuano yote msimu
huu.
Mshindi huyo wa tuzo ya goli bora
(Puskas) la mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 amekosa mechi
nyingi kipindi akiuguza majeraha yake na sasa amesema amerejea kwa kasi
kuisaidia timu yake.
Aidha kuelekea mechi za robo
fainali klabu bingwa dhidi ya Atletico Madrid mwezi ujao hii ni habari
nzuri kwa kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti ambaye amekuwa akimtumia
mcolombia huyo katika nafasi tofauti ndani ya uwanja.
0 maoni:
Post a Comment