Rais wa ligi kuu ya soka nchini
Hispania maarufu kama La Liga amesema kuwa Cristiano Ronaldo naweza
akapata adhabu ya ukosefu wa nidhamu kutokana na aina ya ushangiliaji
aliouonesha katika mechi ya El Classico dhidi ya Fc. Barcelona na hii ni
mara baada ya kusawazisha goli katika mchezo uliochezwa siku ya
Jumapili Nou Camp.
Ronaldo alionekana akitoa
ishara ya kuwataka mashabiki wa Fc. Barcelona watulie mnamo dakika ya 31
aliposawazisha goli hilo kwa upande wa Real Madrid ndani ya El Classico
Camp Nou.
Tebas wakati anaongea na
waandishi wa habari alisema “Inatakiwa tuwe makini sana na ishara za
ushangiliaji pindi mchezaji anapofunga goli au aina yoyoye ile ya
ushaingiliaji wa ishara ambayo inaweza ikachochea vurugu kwa watazamaji”
“Tunaweza kutoa adhabu ya faini au kusimamisha mechi kadhaa, tutaliangalia hili suala”
Mamlaka ya ligi kuu ya Hispania
wamekuwa wakiweka jitihada za ziada kuzuia aina ya ushangiliaji yenye
ishara za ushawishi tangu tangu kufariki kwa mshambuliaji wa Derpotive
La Coruna mwaka jana.
Mnamo mwezi wa 12 mwaka mwaka
jana chama cha La Liga kiliripoti kuwa vilabu vitano Real Madrid, Fc.
Barcelona, Derportive, Rayo Vallecano na Granada kutokana na aina ya
ushangiliaji wa kukera ambapo pia Barcelona waliufanya kwa Cristiano
Ronaldo walipomzomea na wakimuita ni mlevi wakati mchezo unaendelea”
Teabs ambaye alikuwa akiongea
katika seminar huko Barcelona alisema ligi hiyo ni ligi bora duniani na
ilie iendelee kuwa bora ni lazima iwe katika hali ya usalama zaidi hali
ambayo itanyamazisha vilio na vurugu katika mpira.
Wakati huohuo kilabu ya Real
Madrid imemmpiga marufuku moja kati ya mwanachama wake na kuiomba tume
ya nchini humo kufanya uchunguzi kwa mashaiki wengine wawili ambao
walionekana wakiwatukana matusi wachezaji kufutia mchezo wa Jumapili
dhidi ya Barcelona.
Uongozi wa Real Madrid ulisema
mapema jumatatu baada ya kugundua kupitia picha waliweza kumpia marufuku
mmoja kati ya wanachama wao kuingia katika uwanja wa Santiago Bernabeu
pamoja na kumfuta uanachama wa kilabu hiyo au sehemu yoyote ile
itakayohusisha kilabu ya Real Madrid.
0 maoni:
Post a Comment