Wednesday, March 25, 2015


Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati), ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga. akiongea wakati wa tukio la kumuaga na kumkabithi bendera ya taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. pichani katikati ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua akifatiwa na mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi.
mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika bendera mara baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya muziki ya Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika Jumamosi hii nchini Kenya.

Barasa la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.

Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million 50.

Akiongea wakati wa kukabithi bendera hiyo, Mkurugenzi wa ukuzaji sanaa na Masoko wa BASATA bi Nsao Shalua alisema” kwanza tunachukua fulsa kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha shindano hili na kwa kufata taratibu zote za kuratibu mashindano. Airtel leo wameonyesha mfano kwa kumleta mshindi hapa ofisini, kuaga rasmi na kupatiwa kibali cha kusafiri kutoka baraza la sanaa Tanzania kitu ambacho hakifanywi na makampuni mengi na hata wasaani wengi nchini. Huu ni mfano wa kuigwa na natoa wito kwa watu wote wanaoondoka nchini kwaajili ya kwenda kufanya shughuli za sanaa kuhakikisha wanafata utaratibu kwa kutufahamisha na kupata hati maalumu ya kushiriki shughuli na kuiwakilisha nchi yetu nje ya nchi.

Aidha napenda kumpongeza Mayunga kwa kuibuka kuwa mshindi na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika, tunapenda kumwomba atumie fulsa hii vizuri na kwa kufanya hivyo basi tunaamini atafanya vyema. Tunamtakia safari njema na mashindano mema, tunaamini Mayunga atatuwakilisha vyema na kutangaza nchini yetu katika angaza za muziki kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga alisema” Leo tunamuwezesha Mayunga kwenda kushiriki na kuiwakiisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika Tunamwezesha kujiwekea umaarufu na kuonyesha kipaji chake kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na Mayunga tunawawezesha vijana wengi barani Afrika kwa ujumla kuzifikia ndoto zao. Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi , jijini Naivasha Kenya ambapo washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika watachuana vikali. Mshindi wa Airtel Trace Afrika atapata nafasi ya kwenda nchini marekani na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya R&B , Akon na kuweza kurekodi nyimbo zake.

Natoa wito kwa watanzania kumpigia kura Mayunga kwa ku tuma SMS, yaani ujumbe mfupi andika neno YUN kwenda 15594, Alhamisi ni siku ya mwisho ya kupiga kura, asiliimia 25 ya ushindi inatoka kwenye kura yako hivyo kura yako ni ya muhimu sana. Aliongeza Aneth.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa bendera Malimi Mayunga alisema” namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii, nawaahidi watanzania kuwawakilisha vyema, pamoja na hayo nawaomba sana watanzania waniunge mkono kwa kunipigia kura ili nipate nafasi ya kuweza kuibuka kuwa mshindi.

Hii kwangu ni nafasi ya pekee sana na namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha na Airtel kwa kuwawezesha vijana kama mimi kuonyesha vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao kupitia mashindano mengi kama haya Mashindano ya Airtel Trace Music Star yalianzishwa kwa lengo la kuonyesha vipaji vya vijana kimuziki na nakuwapatia fulsa ya kukua kimuziki.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog