Baada
ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na timu za
FFU na Zakhem kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao,kesho
20/03/2015 utapigwa mchezo mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na
mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi ya mikoa.
Mchezo huo wa mtoano
utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za
Pan Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya
pili kwenye makundi yao.
Kwa mujibu wa kamati ya
mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya
kumpata mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa
shirikisho la soka la Tanzania TFF.
Aidha kamati hiyo chini ya
mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza
kwa wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa
Dar es salam tangu ilipoanza kutimua vumbi.
0 maoni:
Post a Comment