Monday, August 10, 2015


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amewashambulia madaktari wa timu yake kuwa ni 'wajinga'' baada yao kutumia muda mrefu kumtibu Eden Hazard uwanjani mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Premia ya Uingereza walipokuwa wakikabiliana na Swansea jana usiku huku wakiwa na mchezaji mmoja zaidi yao.
The Blues, ambao tayari walikuwa keshampoteza kipa Thibaut Courtois aliyekuwa kaoneshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji Bafetimbi Gomis walisalia 9 uwanjani baada ya timu ya utabibu kukimbia kushughulikia mguu wa Hazard na wakachukua muda mrefu japo kulingana na Mourinho hakukuwa 'ameumia sana''

1-1Ayew akipongezwa baada ya kusawazisha ''kwa kweli sikufurahia kauli yao ya kumtibu Hazard,ilitulemaza na kuwapa Swansea fursa ya kutushambuliwa maanake walikuwa na watu wawili zaidi yetu'' alifoka the Special one'' Thibaut Courtois alioneshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji Bafetimbi Gomis ''Hapa uwanjani uwe ni mbeba mpira, daktari ama hata katibu mwandishi sharti uwe unafahamu jinsi mpira unaendelea uwanjani'' ''Kabla ya kuingia uwanjani sharti ufahamu hali halisia kuwa tumekosa mchezaji mmoja na kuingia kutasababisha mwengine aondoke uwanjani''

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog