Leo
Usiku Mabingwa wa zamani wa England Manchester City wanaingia Ugenini
The Hawthorns kucheza na West Bromwich Albion katika Mechi yao ya kwanza
kabisa ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Hii ni Mechi ya mwisho ya Raundi ya
kwanza kwa Timu 20 za Ligi Kuu England ambazo zilianza mbio zao za Msimu
mpya hapo Jumamosi na Jana Jumapili huku ikishuhudiwa Mabingwa Chelsea
kutoka Sare 2 kwa 2 na Swansea City, Man United kuifunga Spurs 1-0 na
Arsenal wakitandikwa kwao Emirates 2-0 na West Ham.Hali za Wachezaji West Brom, chini ya Meneja Tony Pulis, huenda wakamkosa Beki wao ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man City, Joleon Lescott, ambae ana maumivu lakini Wachezaji wao wapya, Rickie Lambert, James McClean na James Chester wapo tayari kucheza isipokuwa Serge Gnabry kutoka Arsenal ambae Uhamisho wake haukukamilika kwa wakati.
Manchester City, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, itawakosa Gael Clichy na Fabian Delph wote wakiwa na maumivu lakini David Silva, Samir Nasri na Sergio Aguero, ambao walikuwa wagonjwa, wako fiti kuanza Mechi hii.
Uso kwa Uso
-Manchester City hawajafungwa na WBA katika Mechi zao 5 zilizopita Uwanjani The Hawthorns, wakishinda 4 kati ya hizo.
-City, wakicheza kwao Etihad na hapo The Hawthorns, wameifunga WBA mara 7 mfululizo.
Mike Dean refa atakayechezesha mpambano huo utakaopigwa usiku huu saa nne kamili kwa saa za hapa Tz.
Referee: Mike Dean Assistants: S Long, M Perry Fourth Official: M Clattenburg
LIGI KUU ENGLAND
Jumatatu Agosti 10
22:00 West Brom v Man City
Ijumaa Agosti 14
22:45 Aston Villa v Man United
Jumamosi Agosti 15
14:45 Southampton v Everton
17:00 Sunderland v Norwich
17:00 Swansea v Newcastle
17:00 Tottenham v Stoke
17:00 Watford v West Brom
17:00 West Ham v Leicester
0 maoni:
Post a Comment