Monday, August 10, 2015

sergio-ramos-cruz-azul-real-madrid-fifa-world-club-cup-12162014_bz7pe05jv18h1haakqqlo63s6

Beki wa kati wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu yake mpaka kufikia alhmis ya wiki hii baada ya kufikia muafaka na uongozi wa klabu hiyo katika mazungumzo ambayo yamedumu kwa muda wa mwezi mzima.
Kusaini kwa mkataba mpya kwa beki huyu kunafikisha ukomo kwa tetesi kadhaa ambazo zilimhusisha na kuihama Real Madrid huku Manchester United ikitajwa kuwa timu ambayo ingemsajili.
Beki huyo ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa Madrid baada ya kuondoka kwa Iker Casillas na kwa nyakati tofauti rais wa klabu Florentino Perez na kocha Rafa Benitez wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa mchezaji huyo kwa timu hiyo na kuwa hatauzwa kwa bei yoyote ile.
Ramos alidaiwa kutoridhishwa na mshahara wa Euro milioni 6 kwa mwaka ambao amekuwa akiupata kiwango ambacho mwakilishi wake na kaka yake Rene Ramos amekuwa akisisitiza kuwa hakilingani na mchango wa beki huyo kwa Madrid katika miaka ambayo ameitumikia .

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog