Friday, August 22, 2014


Pair of aces: Angel Di Maria (left) and Sami Khedira are both on Manchester United's radar
Wote kwenye rada: Angel Di Maria (kushoto) na Sami Khedira wanatakiwa na Manchester United.

MANCHESTER United bado wanapambana kuhakikisha wanawasajili nyota wawili wa Real Madrid, Muargentina, Angel di Maria na Mjerumani Sami Khedira.
Habari njema kwa mashabiki wa United ni kwamba makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward anapigana kuwasajili wachezaji hao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema jumanne kuwa Di Maria na Khedira wanaweza kuondoka.
Di Maria amekuwa katika rada za Louis Van Gaal kwa majira yote ya kiangazi wakati Khedira alimuona wakati anafundisha soka nchini Ujerumani.
Wanted: Di Maria remains a top target for Louis van Gaal and Manchester United this summer
Anawindwa: Di Maria ndiye chaguo namba moja la Louis van Gaal na Manchester United majira haya ya kiangazi.
Open offer: Carlo Ancelotti says ¿if Di Maria doesn¿t find a solution for his future, we would welcome him back'
Milango wazi: Carlo Ancelotti alisema 'kama Di Maria hatapata suluhisho la hatima yake ya baadaye, kwa furaha tutapenda kumkaribisha tena.


MABINGWA wa Bundesliga Bayern Munich wataanza kampeni za kutwaa Taji la Ubingwa wa Germany kwa mara ya 25 wakiwa Nyumbani Allianz Arena Ijumaa Usiku kwa kucheza na Wolfsburg.
Msimu uliopita, wakiwa chini ya Meneja Pep Guardiola, waliweka Rekodi ya kutwaa Ubingwa mapema mno waliposhinda Taji hapo Machi 25 ikiwa karibu Miezi miwili kabla Msimu kumalizika.
Wolfsburg walimaliza Msimu uliopita wakiwa Nafasi ya 5.
Lakini tayari Msimu huu Bayern wameshajeruhiwa baada ya Wiki iliyopita kuchapwa Bao 2-0 katika Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea DFL Supercup huko Signal Iduna Park walipocheza na Mahasimu wao Borussia Dortmund.
Moja ya Mechi kali za Wikiendi ya Ufunguzi wa Msimu wa 2014/15 ni hapo Jumamosi Agosti 23 kwenye mtanange utakaochezwa Signal Iduna Park wakati Borussia Dortmund watakapokuwa Wenyeji wa Bayer Leverkusen.
Dortmund, chini ya Kocha Jurgen Klopp, walimaliza Ligi wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 19 nyuma ya Bayern Munich na wataivaa Bayer Leverkusen ambayo itakuwa chini ya Meneja mpya Roger Schmidt.

BUNDESLIGA
RATIBA
Mechi za Ufunguzi
Ijumaa Agosti 22

21:30 Bayern Munich vs VfL Wolfsburg

Jumamosi Agosti 23
16:30 Hannover 96 vs Schalke 04
16:30 Hertha Berlin vs  SV Werder Bremen
16:30 Eintracht Frankfurt vs SC Freiburg
16:30 FC Köln vs Hamburger SV
16:30 TSG Hoffenheim vs FC Augsburg
19:30 BV Borussia Dortmund v Bayer 04 Leverkusen

Jumapili Agosti 24
16:30 SC Paderborn 07 vs FSV Mainz 05
18:30 Borussia Mönchengladbach vs VfB Stuttgart


Warembo watakaoshiriki mashindano ya Redd's Miss Temeke, wakiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed (TID), anayemiliki bendi ya Top in Town,itakayotoa burudani katika mashindano hayo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed (TID), anayemiliki bendi ya Top in Town, akielezea katika mkutano na waandishi wa habari, katika klabu ya City Sports & Lounge jinsi alivyojiandaa kutoa burudani katika mashindano ya Redd's Miss Temeke yatakayofanyika ijumaa ndani ya TCC Club,Chang'ombe, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwandaaji wa mashindano hayo, Benny Kisaka.Nyuma yao ni baadhi ya warembo watakaoshiriki mashindano hayo.

MALKIA wa kanda ya Temeke, Redds Miss Temeke 2014 anatarajiwa kupatikana Leo Ijumaa Agosti 22, mwaka huu kwenye ukumbi wa TCC Club Chang'ombe. Jumla ya warembo 17 kutoka vitongoji vya Mbagala, Kurasini na Chang'ombe watapanda jukwaani jukwaani kuwania taji hilo.

Alisema kuwa mbali ya shindano hilo kubwa, kulifanyika shindano dogo la awali lililoandaliwa na Michuzi Media Group la Miss Photogenic ambalo mshindi wake atazawadiwa kitita cha Sh. milioni 1 taslimu, shindano ambalo lililsimamiwa na jopo la wapiga picha wa kampuni hiyo ambao watamtangaza na kumpa zawadi mshindi siku ya shindano.

Alisema mkali wa bongofleva, Khalid Mohamed TID almaarufu kama Top in Dar, sanjari na Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania, Young Suma, Super Bokilo na wasanii mbalimbali wanatarajia kupamba shoo hiyo ambayo Dj John Peter Pantelakis atalisindikiza.


Wadhamini wa shindano hilo ni TBL Kupitia Redds wamedhamini shindano hilo sanjari na kinywaji cha Zanzi, Michuzi Media Group, Radio EFM 93.7 Cash & Carry Distributors, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, CXC Africa, 88. 5 Clouds FM, City Sports Lounge, Gazeti la Jambo Leo, Kiwango Security na 100.5 Times FM.

BMP Promotions imeshakamilisha shindano hili la 19 tangu kuanzishwa Miss Temeke chini ya undaaji wake kwa asilimia kubwa, hivyo washabiki wa Kanda ya Temeke na vitongoji vyake watarajie mabadiliko makubwa katika aina ya shindano la urembo litakavyokuwa Ijumaa.


1996- Asela Magaka 1997- Miriam Odemba 1998- Khamisa Ahmed (Miss Temeke anayeendea kujiita hivyo huko Marekani) 1999- Ediltruda Kalikawe 2000- Irene Kiwia 2001- Happyness Sosthnes Magesse super model Millen( Miss Tanzania) 2002- Regina Mosha 2003- Hawa Ismail ( Sylvia Bahame first runner up and Miss Tanzania same year) 2004- Cecylia Assey ( mrs Agrey Marealle), first runner up Miss Tanzania


2005- Seba Aggrey 2006- Jokate Mwegelo (Miss Tanzania fisrt runner up), Irene Uwoya 1st runner Temeke & 3rd runner up Miss Tanzania


2007- Queen David ( Miss Tanzania second runner up)

2008- Angela Lubala (top five Miss Tanzania)
2009- Sia Ndaskoy (top five Miss Tanzania)
2010- Genevieve Mpangala ( Miss Tanzania)
2011- Husna Twalib
2012- Edda Sylvester

runner up Miss Tanzania)

Thursday, August 21, 2014


I'm out: Tim Sherwood has announced that he will not become the next Crystal Palace manager on Thursday
Mimi sipo!: Tim Sherwood jana ametangaza kuwa hatakuwa kocha Crystal Palace .

TIM Sherwood amejitoa mwenyewe katika mbio za kuwa kocha mpya wa Crystal Palace.
Kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Selhurst Park baada ya Malky Mackay kuondolewa katika kinyang'anyiro.
Lakini Sherwood hajavutiwa kurithi mikoba ya kocha aliyeondoka Tony Pulis, na hii inamaanisha Keith Millen ataendelea kuiongoza timu hiyo kwa muda katika mechi ijayo ya ligi kuu dhidi ya West Ham uwanja wa nyumbani.
No go: Sherwood is said to be uninterested in the job and has confirmed he will not take over as manager
Siendi: Sherwood anasema hajavutiwa na kazi hiyo na amethibitisha kuwa hatarithi mikoba.
"Palace ni klabu kubwa yenye utamaduni wake, lakini ipo katika hali ngumu ambayo haiwezi kuonekana kirahisi," Sherwood aliwaambia Sky Sports.
Makubaliano binafsi baina ya Sherwood na Palace yalishindwa kufikia muafaka baada ya kuripotiwa kuwa kocha huyo alitaka kuwa pamoja na wasaidizi wake wakati akiwa Spurs,  Chris Ramsey na Les Ferdinand katika dimba la Selhurst Park.
Mmiliki wa Palace, Steve Parish aligoma mapendekezo hayo na sasa anaangalia uwezekanao wa kupata kocha mpya zikisalia saa 48 tu klabu hiyo ijitupe uwanjani katika mchezo wa ligi kuu.


Na Adam Mbwana, Dar es salaam
Ilikuwa ni vita kali kati ya mafahali wawili ambao naweza kusema kila mmoja wao alikuwa na azimio tofauti kichwani mwake juu ya mwenzie. Vita hii huwezi kuifananisha na na zile za mwaka 1914 na 1939 ambazo ndio vita kubwa kuwahi kutokea duniani pale ambapo mataifa makubwa yalikuwa yalikuwa yakiwania utajiri kwa kutumia silaha kali na hatari duniani, lakini pia vita hii huwezi kuifananisha na ile maarufu ya miaka ya 1960 kati ya Urusi na Marekani wataalamu wakiita vita baridi ambayo haikutumia silaha kama sehem ya mapigano bali silaha ikitumika kama sababu kubwa ya vita hiyo
Lakini vita hii ni tofauti kabisa kwani inapiganwa katika mji ambao hauonekani kwa macho huku vyombo vya habari vikitujuza uwepo wake wakati wahusika wake wakuu wakiwa ni Romelo Lukaku na Josee Mourinho vita ambavyo havikuhitaji usuluhishi bali kuisha kwake kulihitaji mmoja wao akubali masharti ya mwenzake au kama si hivyo basi ilihitaji watu hawa kutengana kwa muda kama sio moja kwa moja.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho

Wahusika hawa walikuwa na mawazo tofauti vichwani mwao, Lukaku akihitaji kuhakikishiwa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Chelsea huku Mourinho naye akimtaka Lukaku apiganie nafasi yake katika timu mbele ya washambuliaji wengine kwenye timu kama Fernando Torres, Diego Costa na Didier Drogba. Na hapo ndipo vita iliponoga zaidi.
Tangu kusajiliwa kwake Chelsea August 2011 akitokea katika klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji kwa paundi milion 17,  Romelo Lukaku ameshindwa kabisa kuonyesha uwezo mkubwa katika klabu hiyo ya Chelsea kama ambavyo wengi walitegemea.
 Wengi walidhania kuwa Lukaku ndiye atakuwa mrithi sahihi wa Didier Drogba katika safu ya ushambuliaji ya Chelsea kutokana na ukweli kwamba wawili hawa wanafanana sana kwa maumbo yao makubwa, staili ya kucheza kwa kutumia nguvu na hata kuwa na uwezo wa kuhimili beki zaidi ya mmoja. 
Diego Costa

Lakini hata hivyo mshambuliaji huyo mzaliwa wa Anrwerp nchinj Ubelgiji alimaliza msimu wake wa kwanza darajani akiwa mchezaji wa kikosi cha akiba.
Hali hiyo ilimfanya kupelekwa kwa mkopo msimu uliofuata wa mwaka 2012 katika timu ya Westbromwich Albiol ambapo aliweza kufunga magoli 17 na kumaliza katika nafasi ya sita ya wafungaji bora wa ligi kuu ya uingereza kwa msimu huo. Msimu uliofuata wa 2013-2014 alipelekwa tena kwa mkopo katika klabu ya Everton ambapo ambako nako alizifumania nyavu mara 15  katika mechi 31 alizocheza na kuisaidia Everton kumaliza katika nafasi ya 5 ya ligi huku akiwa na uwiano mzuri wa magoli zaidi ya washambuliaji wa chelsea Fernando Torres, Samuel Eto'o na Demba Ba ambao kwa pamoja waliweza kufunga magoli 19 tu.
Maneno yalianza kuibuka katika vyombo vya habari huku wachambuzi wa soka wakihoji nafasi ya Lukaku katika safu ya ushambuliaji ya Chelsea ambayo ilionekana kupwaya msimu uliopita chini ya kocha Josee Mourinho ambaye mara kwa mara alikuwa akiwalalamikia washambuliaji wake hao kwa kushindwa kuzifumania nyavu mara kwa mara.
Didier Drigbo amerudi Chelsea

Wachambuzi hao walimpa Lukaku sababu ya kuanza kudai nafasi ya kudumu katika kikosi cha Chelsea baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo na Everton huku Mourinho akiweka pamba msikioni na kuendelea na mpango wake wa kumsajili mshambuliaji Diego Costa kutoka Atletico Madrid baada ya kuondoka kwa Samuel Eto'o na Demba Ba.
Kwa Lukaku hizi zilikuwa ni habari mbaya sana na ikawa ni moja ya sababu kubwa ya kuchochea vita kati yake na Mourinho kwani yeye alitegemea baada ya kuondoka kwa Etoo na Ba kungempa yeye nafasi ya kurudi kuchukua nafasi yake aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu lakini badala yake akaletewa kipingamizi kingine ambaye ni Costa huku Mourinho akimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kumwambia kuwa apiganie nafasi yake. Lakini kilichommaliza nguvu kabisa Lukaku na kurejea kwa Drogba klabuni hapo. Hapo ndipo Mourinho akamthibitishia Lukaku hakumuhitaji tangu mwanzo. Kwahiyo Lukaku alishuhudia makombora na vifaru vya kivita vikiingia kwenye ghala la silaha la Mourinho huku naye akishuhudia kwa macho yake.
Hatimaye Lukaku yakamshinda baada ya kuona adui yake hawezekaniki. Sasa ameamua kubwaga manyanga na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusalimu amri baada ya kukamilisha usajili wake wa kudumu katika klabu ya Everton wenye thamani inayotajwa kufikia paundi million 28.
Lakini suala la msingi la kujiuliza hapa ni Je, Mourinho alikuwa anataka nini cha ziada kutoka kwa Lukaku ili aweze kumpa nafasi? na Je, madai ya Mourinho kuwa Lukaku hakutaka kugombania nafasi kikosini ni ya kweli au ni kujisafisha tu mbele ya vyombo vya habari? na swali la mwisho ni Je, kwanini Torres abaki kikosini na kumuuza Lukaku ambaye msimu uliopita amefanya mambo makubwa zaidi ya Torres licha ya kuwa na umri mdogo?

Waswahili husema "funika kombe mwanaharamu apite". Hicho ndicho alichokifanya Lukaku baada ya kuamua kukubali kushindwa dhidi ya Mourinho. Ameamua kuanza maisha mapya Everton huku akimuacha Mourinho na pamba zake masikioni. Ama kweli asiyekubali kushindwa sio mshindani.

 

Mshiriki Nambari 1 (Subira Ally).
Mshiriki Nambari 2 (Hellen Eugen).
Mshiriki Nambari 3 (Rehema Jabiry).
Mshiriki Nambari 4 (Catheline Alex).
Mshiriki Nambari 5 (Dalena David).
Mshiriki Nambari 6 (Winfrida Guntram).
Mshiriki Nambari 7 (Salama Salehe).
Mshiriki Nambari 8 (Magdalena Majawa).
Mshiriki Nambari 9 (Grace John).
Mshiriki Nambari 10 (Lilian Loth).
Mshiriki Nambari 11 (Amina Salum).
Mshiriki Nambari 12 (Rebeca Mdamu).
Mshiriki Nambari 13 (Sitti Mtemvu).
Mshiriki Nambari 14 (Ellen Sule).
Mshiriki Nambari 15 (Neema Mollely).
Mshiriki Nambari 16 (Lucy Lewis).
Mshiriki Nambari 17 (Esther Mnahi).

 


Wachezaji wa Coastal Union wakiwa uwanja wa ndege Tanga wakipanda ndege kuelekea Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania bara, safari hiyo imedhaminiwa na wafadhili wa timu hiyo
kiwanda cha Unga mkoani Tanga Pembe..


.

waliotembelea blog