Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia Taifa Stars, Farouk Baghouza amewaomba Watanzania kujitokeza na kuichangia kamati yake ili iweze kufanikisha lengo la kuisaidia Stars.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, pamoja na kutangaza kamati kubwa na ndogondogo kwa
ajili ya kuisaidia Stars, Farouk alisisitiza suala la Watanzania kujitolea.
“Mwenye
maji, mwenye dawa tunakaribisha michango. Lengo ni kuisaidia timu, lakini lengo
ni kuonyesha umoja na utaifa wetu.
“Taifa
Stars inatuwakilisha Watanzania wote hata wasio wapenda soka, tafadhari
tuungane pamoja katika kipindi hiki kuhakiksha tunaing’oa Algeria,” alisema.
Stars
inakutana na Algeria Novemba 14 katika mechi ya kwanza iatakayochezwa jijini
Dar es Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17 nchini Algeria.
Mechi hiyo
ni ya kuwania kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Stars
imepata nafasi hiyo baada ya kuing’oa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1 ikiwa
imeanza na ushindi wa mabao 2-0 jijini Dar es Salaam, ikapoteza 1-0 mjini
Blantyre.
Algeria
ndiyo timu bora kuliko zote Afrika, pia ndiyo timu ya Afrika iliyofanya vizuri
zaidi katika michuano ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Brazil, mwaka jana.
0 maoni:
Post a Comment