Mwandishi wa Gazeti la Championi, Nicodemus Jonas wa
pili kulia akiwa na vyeti alivyochukuwa kwa niaba ya Blog ya Salehjembe na
Kampuni ya Global Publishers vilivyotolewa na Asasi ya Somi katika Tamasha la
Majimaji Selebuka. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza wa Asasi ya Somi, Prof. Julian
Murchison, Dk Damas Ndumbaro- mkurugenzi mwenza wa Somi na Mkuu wa Jumba la
Makumbusho mjini Songea, Balthazar Namusya.
Katika kule kilichoonekana Blogu ya Saleh Jembe ndiyo blog pendwa kwa michezo nchini,
imetunukiwa cheti na Asasi ya Songea –Mississippi (Somi) kwa kutambua mchango
wake katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, lililohitimishwa juzi Jumamosi.
Tamasha
hilo lililenga kudumisha uhusiano wa Jimbo la Songea na Mississippi ya nchini
Marekani kiuchumi kwa kuwaninua wajasiriamali pamoja na kudumisha sekta ya
michezo mkoani Ruvuma.
Akizungumza
wakati wa kufunga tamasha hilo, kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita
vya Majimaji mjini Songea, Mkurugenzi Mwenza wa Somi, wakili Dk Damas Ndumbaro
alisema: “Saleh Jembe blog ilikuwa bega kwa bega nasi, mwanzo mpaka mwisho wa
tamasha hilo.
“Tunashukuru
watu wengi wamehamasika na wamekuwa wakitufuatilia kupitia blogu hii, hivyo ni
lazima tulipe fadhaira kwake.”
Tovuti na
Global Pulishers, nayo ilitunukiwa cheti kama hicho kwa sapoti ya kuripoti
matukio yote yaliyojili kwenye tamasha hilo, ambayo ni: Riadha, maonyesho ya
ngoma za asili, maonyesho ya wajasiriamali, mbio za baiskeli pamoja na utalii
wa ndani.
|
0 maoni:
Post a Comment