MABINGWA
wa Italy Juventus wamteua Massimiliano Allegri kuwa Kocha wao mpya
ikiwa ni Siku moja tu tangu Antonio Conte aamue kuondoka. Jana, baada
kuiongoza Juve kwa mafanikio makubwa katika Misimu Mitatu, Conte aliamua
kuachana na Klabu hiyo kwa mshangao wa wengi.
Afisa Habari wa Juve, Gabriella Ravizzotti, amesema kuwa Allegri atatambulishwa rasmi Leo Mchana.
Inaaminika Allegri amekubali kusaini Mkataba wa Miaka Miwili na atalipwa Euro Milioni 2 kila Msimu.
Allegri, mwenye Miaka 46, amekuwa hana kazi tangu atimuliwe na AC Milan Januari Mwaka huu baada kufanya vibaya lakini hilo halikuwatisha Juve katika kumteua.
Kocha huyo alijiunga na AC Milan Mwaka 2010 akitokea Cagliari ambako alikaa kwa Miaka miwili na kuwapa mafanikio makubwa.
Conte alijiunga na Juve kutoka Siena Mwaka 2011 na kuipa Juve Ubingwa mara 3 mfululizo ikiwa pamoja na Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wakizoa Pointi 102 na kuwa Timu ya Kwanza Italy kuvuka Pointi 100.

0 maoni:
Post a Comment