Salamu: Van Gaal (katikati) amekutana na msaidizi wake Ryan Giggs (kushoto) na makamu mwenyekiti Ed Woodward.
Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 2:14 usiku
KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Carrington leo jumatano kuanza kazi yake mpya.
Mholanzi huyo alipigwa picha akiwa geti
kubwa, lakini baadaye klabu iliposti picha katika mtandao wake wa Twita
akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Van Gaal alitaka kuonana na wachezaji wake baada ya kombe la dunia pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Van Gaal amerudi baada ya kuiongoza Uholanzi kushika nafasi ya tatu ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Majadiliano: Giggs, Van Gaal na Clive Woodward wana kibarua kikubwa cha kuirudisha United katika hadhi yake.
Van Gaal ametua kazini siku nne tu tangu aiongoze Uholanzi kushika nafasi ya tatu na kwa maana hiyo amejinyima mapumziko.
Kocha huyo mwenye miaka 62, ni kocha wa
kwanza kuiongoza Man United kutoka nje ya British,na hatakuwa na muda wa
kupoteza katika harakati zake za kuijengga United.
Kesho alhamisi, atatangazwa rasmi katika
mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari ya
kwenda nchini Marekani kuweka kambi ya maandilizi ya kabla ya msimu.
United itacheza mechi dhidi ya Los
Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real Madrid, wakati mechi ya
kwanza ya Van Gaal katika dimba la Old Trafford itakuwa ya kirafiki
dhidi ya Valencia Agosti 12 mwaka huu.
Siku nne baadaye United wataanza ligi kuu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Swansea.
Watu wa kazi: Giggs (kushoto) na Van Gaal watafanya kazi pamoja kufuta majanga ya David Moyes msimu uliopita.
0 maoni:
Post a Comment