Ander Herrera alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal kwa dau la puandi milioni 28.4
Imechapishwa Julai 17, 2014, saa 5:27 asubuhi
Nicky Butt amemtabiria Ander Herrera
kupata mafanikio katika klabu ya Manchester United, lakini amekiri kuwa
Mhispania huyo hawezi kuwa katika kiwango kimoja na wachezaji kama Toni
Kroos au Paul Pogba.
Nyota huyo mwenye miaka 24 alikuwa wa kwanza kusajiliwa majira haya ya kiangazi na kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal kutokea klabu ya Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 28.4 .
Wakat huo huo, mchezaji aliyekuwa
akiwindwa na Manchester United, Kroos yupo katika hatua za mwisho
kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Real Madrid.
Naye mchezaji aliyeibukia kutoka akademi
ya Man United, Pogba amewekewa ngumu kutoka Juventus ambapo imekaririwa
kuwa kama timu inataka saini yake lazima iguse mfuko na kulipa dau nono
la paundi milioni 60.
Herera hawezi kuwa katika kiwango cha Toni Kroos4
Ander Herrera hawezi kuwa katika kiwango sawa na Paul Pogba.
Butt, ambaye kwasasa ni miongoni mwa
watu wanaounda benchi la Ufundi la Old Trafford, amekiri kuwa Herera
anahitaji muda kufikia kiwango cha wapinzani wake.
"Herera hakuwa katika kiwango kikubwa
sana, lakini tulilazimika kumchukua kwasababu hakukuwepo na viungo wa
kiwango cha juu zaidi,". Alisema Butt.
0 maoni:
Post a Comment