Dili limakamilika: Toni Kroos amesaini
mkataba na klabu ya Real Madrid kwa dau la paundi milioni 24 kutokea
klabu ya Bayern Munich
TONI Kroos amekamilisha uhamisho wa
paundi milioni 24 kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kutoka
kwa mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.
Mabingwa hao wa Ujerumani wametangaza
leo asubuhi kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili na nyota huyo
anaondoka muda wowote.
Mkataba wa Kroos ulikuwa unamalizika
majira ya kiangazi mwakani na mshindi huyo wa kombe la dunia amesaini
mkataba wa miaka sita katika dimba la Santiago Bernabeu.
0 maoni:
Post a Comment