Historia ya Klabu ya Simba Tangu 1920 hadi 2014
Mwandishi: Mwina Kaduguda
Mchapishaji: Mkuki na Nyota Publishers
Mwaka: 2014
Kurasa: 128
Bei: Shilingi 15,000/=
Muhtasari wa Kitabu
Hiki ni kitabu cha kwanza chenye historia ya kina ya Simba Sports Club.
Kama mpenzi wa soka, hususan mkereketwa wa Simba, utajua chimbuko na
undani wake tangu ilipoanzishwa hadi hii leo. Vilevile utaweza kutumia
kitabu hiki kama ushahidi katika mabishano na mijadala inayohusiana na
klabu, wachezaji, viongozi, timu pinzani na bila kusahau historia ya
soka la Tanzania kwa ujumla.
Utasoma vioja vya soka letu kama
vile ushabiki wa kupindukia, vituko na imani za kishirikina, makundi
yaliyotia fora, migogoro, mafanikio, picha za matukio mbalimbali, bila
kusahau rekodi za mwenendo wa timu na misimamo ya ligi katika historia ya klabu.
Kwa kukisoma kitabu hiki utafahamu
pia mambo mengi yanayolizunguka soka la Tanzania, kwani rekodi hizi
hazipatikani kwa urahisi na mwandishi ametumia muda mwingi kufanya
utafiti na kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali rasmi kama vile
maktaba, vitabu, magazeti, nyaraka na kuwahoji wazee wa zamani. Kwa
mfano, utajua ni lini soka liliingia na kusambaa nchini katika karne ya
20, mpasuko uliozaa Simba na Yanga na mengine mengi ya kuburudisha, kuelimisha na kusisimua.
Kuhusu Mwandishi
Mwina Mohamed Seif Kaduguda,
mzaliwa wa Kasulu, Mkoa wa Kigoma ana shahada ya Bachelor of Arts (B.A.
Hons), Ushirikiano wa Kimataifa na Utawala, UDSM 1992, Cheti cha
Uandishi wa Habari-TSJ, 1994. Ana Diploma ya Ukocha wa Soka
HUPE-Budapest, Hungary 1997, Cheti cha Utawala wa michezo-IOC, 2001,
Cheti Cha Uamuzi wa Soka-FRAT, 2001 na Cheti Cha Juu cha Ukocha-CAF,
2006.
Ameshika nafasi nyingi za uongozi
wa Mpira wa Miguu nchini zikiwamo zile za Katibu Mkuu FAT sasa TFF,
2003–2004, Katibu Mkuu TAFCA, 2002–2008, Katibu Mtendaji SPUTANZA,
2001–2004, Katibu Mkuu TASWA, 1997–2004 Mkufunzi Msaidizi wa Makocha wa
soka TFF, 2006, Katibu Mkuu SIMBA S.C., 2006–2010 na Mjumbe BMT,
2000–2005. Ameshiriki katika makongamano ya kimataifa ya michezo
Toronto-Canada, Athens-Ugiriki, Kuala Lumpur-Malaysia na Sandton
City-Afrika ya Kusini.
Hivi sasa ni mwalimu katika Shule
ya Sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam na anapatikana kwa mahojiano na
majadiliano kuhusu mada mbalimbali zilizomo kitabuni.
KWA TAARIFA ZAIDI AU MANUNUZI YA JUMLA NA REJA REJA WASILIANA NA:
Mkuki na Nyota Publishers Ltd
Simu: 0787558448
Pepe: buy@mkukinanyota.com
24, Samora Ave, Dar es salaam.
TPH Bookshop (Dar es Salaam)
Simu: 0687238126
24, Samora Ave, Dar es salaam.
TPH Bookshop (Dodoma)
Tel: 0783446790
Pepe: sipho@tphbookshop.com
Gorofa ya Pili, Jengo la Chimwaga, UDOM–Dodoma
Pia kinapatikana katika maduka ya
vitabu na stendi za magazeti mbalimbali nchini. Pata nakala yako sasa!
Bei ya rejareja ni Shilingi 15,000/= tu.
0 maoni:
Post a Comment