Baada
ya kufululiza kwa matokeo mabaya dhidi ya Chelsea na Norwich, kocha wa
Man city, Manuel Pellegrini ameamua kuwaita mazoezini wachezaji wake
wote walikuwa majeruhi na wazima ili kurudisha hali ya timu kabla ya
mambo kuharibika. Man city inakabiliwa na majeruhi wengi wakiwemo
wachezaji tegemezi kama Fernandinho, Samir Nasri na Sergio Aguero.
Licha ya kuwa majeruhi wachezaji hawa wameonekana kwenye mazoezi leo
asubuhi na wanatarajiwa kuanza kucheza hivi karibuni ili kurudisha
kiwango cha timu na kuendelea kucheza kiushindani. Mechi zijazo za Man
city ni dhidi ya Sunderland, Chelsea (FA), Barcelona (UEFA) na Stoke
City.
0 maoni:
Post a Comment