Mechi
ya ligi kuu ya Premier kati ya Fulham na Liverpool siku ya Jumatano,
huenda ikahairishwa ikiwa mgomo wa wafanyakazi wa treni mjini London
utaendelea kama ulivyopangwa. Wafanyakazi hao wa treni wanatarajiwa
kuanza mgomo wa saa 48 kuanzia leo, hali ambayo inaweza kutatiza
shughuli za usafiri kama ilivyokuwa wiki iliyopita mjini humo.
Wasimamizi wa Fulham wana wasi wasi kuwa wafanyakazi wao huenda
washindwe kufika kazini kwa muda unaofaa au hata kukoza kufika ili
kuhakikisha kuwa mechi hiyo imeendelea. Klabu hiyo inatarajiwa kutangaza
baadaye hii leo ikiwa mechi hiyo itahairishwa au la. Wamiliki wa klabu
hiyo wamekuwa na mazungumzo na maafisa wa baraza la mji wa London pamoja
na maafisa wa polisi na wamesema kuwa wana matumaini kuwa mechi hiyo
itachezwa kama ilivyopangwa. Huku hayo yakijiri, leo hii kutakuwa na
mechi kadhaa za ligi kuu ya premier. Cardif City itakuwa mwenyeji wa
Aston Villa, Southampton kusafiri ugenini kucheza na Hull City. West Ham
itakuwa nyumbani kutoana jasho na Norwich, ili hali West Brom kualika
vinara wa ligi hiyo kwa sasa Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani.
0 maoni:
Post a Comment