7:03 AM
Unknown
Katika umri wa miaka 76 amekuwa jina linatamba na nyota wa kurasa za mbele za majarida.
Lakini Papa
Francis kwa sasa anapambana kwa nguvu zote kuepuka kuwa mtu maarufu -
ameamuru kuondolewa kwa sanamu yake kwenye kanisa kuu la mjini Buenos
Aires.
Tangu kusimikwa kwake waumini wamekuwa
wakitembelea sanamu hiyo iliyoko katika bustani ya kanisa kutoa heshima
kuu kwa baba mtakatifu huyo, wakati watalii wamekuwa wakipiga picha
kando yake.
Lakini Papa Francis, Askofu wa zamani wa mji mkuu huo wa Argentina, aliripotiwa kutishwa na habari hizo.
Alipiga
simu moja kwa moja na kutoa maneno makali kwa padri huyo aliyehusika
akimweleza: "Angusha hicho kitu, haraka", gazeti la Argentina la Clarin
liliripoti.
Vyanzo vya kanisa vililieleza gazeti hilo kwamba Papa
Francis amedhamiria kuepuka kutengeneza 'upendo wa ubinafsi' kama ule
aliofurahia Papa John Paul II.
Tangu alipochaguliwa mwezi Machi, Papa
Francis amefika mbali kuonekana kama asiyetaka makuu, akionesha
uvumilivu kidogo kwa ufahari na msukosuko unaokuja na nafasi yake kama
kiongozi wa Wakatoliki bilioni 1.2 kote duniani.
Mara chache huvaa
joho na mapambo ya kitamaduni maalumu kwa Papa huyo, na kuendelea badala
yake kuvalia kanzu ya kawaida nyeupe na msalaba wa chuma.
Amegoma
kuhamia kwenye makazi ya kifahari ya Papa, akisema ni makubwa mno, na
kupenda kuishi badala yake katika nyumba ya kawaida ya wageni kwa ajili
ya watawa wanaokuja kutembelea Vatican., ambao pamoja nao hula chakula
na kuendesha misa kila siku asubuhi.
Lakini umaarufu wake mpya
hauepukiki - hasa kuondoshwa kwa sanamu hiyo kugongana na kutajwa kwa
Francis kama Mwanaume Bora wa Mwaka na jarida la Vanity Fair
lililochapishwa Italia.
Jarida hilo lilisema: "Siku zake 100 tayari
zimemweka kwenye kundi la viongozi wa dunia walioweka historia. Lakini
mapinduzi yanaendelea..."
Sanamu hiyo, iliyosimikwa siku kumi
zilizopita, ilikuwa ni mtazamao wa mchongaji Fernando Pugliese, ambaye
pia alitengeneza sanamu bustani ya wazo Katoliki inayoitwa Holy Land
(Ardhi Takatifu) nchini Argentina. Hapo awali alishawahi kutengeneza
sanamu za Papa John Paul II na Mama Teresa.
Inasubiriwa kuona kama
makumbusho ya Papa Francis kwenye eneo hilo, yaliyotangazwa wiki mbili
zilizopita, nayo yatapigwa marufuku na Papa huyo.
0 maoni:
Post a Comment