SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza
jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema
kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.
“Kupitia
wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na
ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato
kupitia kadi za simu”alisema.
Alisema
katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh
1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana
serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze
kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh
12,000.
Alisema
baadae serikali ilipokea mapendekezo mbalimbali ili kuangalia kama hilo
linaweza kutekelezeka na walipita ngazi zote kabla halijapelekwa katika
kamati za Bunge na kushauriwa kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa
lengo la kukuza uchumi hasa maeneo ya vijijini.
“Tathmini
zote zimefanyika kikamilifu na baadae suala hilo likafikishwa Bungeni
ambapo pia napo lilikubalika... inawezekana watu wanalalamika lakini
ngazi zote suala hilo lilipopita lilikubalika na ikaonekana ni sawa
kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya simu” alisema.
Alisema
kutokana na hilo kwa kutwa nzima kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au Sh
100 kwa siku tatu ambapo serikali inaangalia utaratibu mzuri ambao
hautamuumiza mtumiaji wa simu.
Dk
Mgimwa alisema fedha hizo zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji wa
maji vijijini, umeme pamoja na kuboresha miundombinu katika maeneo ya
vijijini.
0 maoni:
Post a Comment