STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel juzikati alifunguka na kuweka wazi
juu ya mipangilio yake ya ndoa kuwa anatarajia kubeba ujauzito siku
chache zijazo kwani ana kiu kubwa ya kuitwa mama.
Akichonga
na paparazi wetu Julai 9, mwaka huu nyumbani kwake Mwananyamala jijini
Dar, Aunt alisema kuwa anajutia sana kukaa kwa muda wote bila kuiruhusu
mimba iingie ila siku si nyingi mambo yatakuwa yametiki.
“Nina mpango
wa kubeba mimba na nizae siku chache zijazo kwani sina sababu tena ya
kunifanya nisipate mtoto kwa wakati huu ambao niko ndani ya ndoa na
naamini itaimarika zaidi nikiitwa mama huku pembeni akiwepo baba wa
mtoto wangu,” alisema Aunt Ezekiel.
0 maoni:
Post a Comment