Friday, August 22, 2014

MMGM3002
Mshindi wa taji la Miss Temeke 2014,Sitti Mtemvu akipungia mkono mara tu baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndie aliestahili kupata taji hilo katika shindano lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa TCC Club,Chang’ombe jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mshindi wa pili,Salama Saleh na kulia ni Mshindi wa tatu,Neema Mollely.PICHA KWA HISANI YA MICHUZIBLOG
MMGM2844
Mwanalibeneke Othman Michuzi akimvisha taji la Michuzi Blog Miss Photogenic 2014 Mrembo Lilian Loth (9) kwa niaba ya Ankal,baada ya kuonekana ndie Mrembo pekee mwenye mvuto wa picha katika shindano la Miss Temeke 2014,lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa TCC Club,Chang’ombe jijini Dar es salaam
MMGM2906
Baadhi ya Warembo wa Miss Temeke 2014 wakiongozwa na Michuzi Blog Miss Photogenic,Lilian Loth wakiwa kwenye picha ya pamoja kusubiria kutangazwa mshindi wa jumla wa shindano hilo.

IMG_2829
Kikundi cha Platinum Dancers kikionyesha umahiri wao wakati wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta, lililofanyika katika Ukumbi wa Klabu Lavida , mjini Tanga leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Serengeti fiesta linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 23 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
IMG_2830
Majaji wa shindano la kumsaka mshindi wa  dansi la Serengeti fiesta wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyotoana jasho ili kumpata mshindi wa shindano hilo.
IMG_2831
Kundi la Street Color, likionyesha umahiri wao katika  kinyang’anyiro hicho ambacho  mshindi aliondoka na kitita cha sh milioni  moja na kupata nafasi ya kutoa shoo katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
IMG_2832
Lucas Kaili wa kundi la Ice Cream naje akijaribu bahati yake wakati wa shindano hilo. 
IMG_2833
Kundi la Ice Cream likipozi kwa picha mara  baada ya kutangazwa  washindi wa dansi la Serengeti fiesta na kujishindia  zawadi ya sh milioni moja.


 

 Kocha Jose Mourinho akizungumza na Waandishi wa habari na akisema kuwa tayari wapo tayari na wako fiti kuikabiri Leicester.


Eden Hazards na Filipe Luis wakikabana leo kwenye mazoezi yao ya mwisho Stamford Bridge tayari kwa kuikaribisha timu iliyopanda Daraja msimu huu Leicester
Jon Obi Mikel na Mohamed Salah kwenye mazoezi leo huku Viongozi pamoja na Meneja Jose akiwaangalia..
Salah, Luiz na Hazard wakifanya mazoezi kwenye uwanja wao wa Nyumbani Stamford Bridge

Diego Costa, Nathan Ake, Oscar na Mikel


LA LIGA
RATIBA
Mechi za Ufunguzi
Jumamosi Agosti 23

20:00 Malaga CF v Athletic de Bilbao
22:00 Sevilla FC v Valencia
22:00 Granada CF v Deportivo La Coruna
2359 UD Almeria v RCD Espanyol
 

Jumapili Agosti 24
20:00 SD Eibar v Real Sociedad
22:00 FC Barcelona v Elche CF
22:00 Celta de Vigo v Getafe CF
23:59 Levante v Villarreal CF

Jumatatu Agosti 25
21:00 Real Madrid CF v Cordoba
23:00 Rayo Vallecano v Atletico de Madrid

Ijumaa Agosti 29
21:00 Getafe CF v UD Almeria
23:00 Valencia v Malaga CF


 
Kocha Msaidizi wa Tanzania XI, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ (kushoto) akizungumza na nyota wa zamani wa Real Madrid, Fernando Sanz Duran. 
 Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo akizungumza na waandishi wa habari jana (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni nyota mwingine wa Real Madrid, Christian Karembeu na katikati ni mratibu wa ziara ya wanasoka hao, Mkurugenzi wa Kampuni ya TSN, Farough Baghozah.


Heading for Merseyside? Former Chelsea striker Samuel Eto'o could be set to sign for Liverpool
Anakwenda Merseyside? Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o anaweza kujiunga na Liverpool.

MCAMEROON, Samuel Eto'o yuko tayari kukamilisha usajili wa ghafla kujiunga na Liverpool.
Mario Balotelli aliwasili Merseyside jana kujaribu kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 16 kujiunga Anfield, lakini kama dili litashindikana, nafasi yake itachukuliwa na Mcameroon.
Inafahamika kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alipimwa afya na Liverpool akiwa mjini Paris jana ijumaa.
Eto'o mwenye miaka 33 ambaye anaishi mji mkuu wa Ufaransa, amekubali dili la miezi 12 (mwaka mmoja) kujiunga na Liverpool na anasubiri kupanda ndege kwenda kusaini mkataba.
Eto’o aliripotiwa kuvutiwa na Everton kwa siku chache zilizopita, lakini kigezo cha kucheza ligi ya mabingwa kimemfanya aichague Liverpool.
Mersey paradise: The Cameroon striker, pictured here at the World Cup, was also linked with Everton
Picha hii ya Mcameroon huyu alikuwa katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.


Na Baraka Mpenja
NUSU fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe ka Kagame iliendelea jana mjini Kigali, nchini Rwanda na kupata klabu mbili za kucheza fainali na hatimaye kupatikana bingwa atayechukua kombe lililoachwa na Vital’O ya Burundi.
Katika nusu fainali ya kwanza, El Merreikh ya Sudan ilitinga fainali baada ya kuifunga KCC ya Uganda kwa penalti 3-0.
Mshindi alipatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati kufuatia dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika nusu fainali ya pili, APR walikutana na Wanyarwanda wenzao, timu ya Polisi.
Maafande wa APR walitinga fainali baada ya kushinda kwa penalti 4-3 kufuatia suluhu pacha ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
Katika hatua ya robo fainali iliyomalizika juzi katika uwanja wa Nyamirambo, mechi moja tu ndio ilimalizika ndani ya dakika 90 baina ya KCC ya Uganda na Altabara ya Sudan Kusini.
Mechi ya Azam fc dhidi ya El Merreikh alimalizwa kwa penalti ambapo Wasudan waliibuka na ushindi wa penati 4-3 kufuatia dakika 90 kuhitimishwa kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
Robo fainali nyingine iliwakutanisha Atletico ya Burundi dhidi Polisi ya Rwanda.
Polisi walishinda kwa penalty 9-8 kufuatia suluhu ya bila kufungana katika dakika 90, lakini rekodi iliyowekwa ni wachezaji wote 22 kupiga penalti.
Robo fainali nyingine iliyohitimishwa kwa mikwaju ya penalti ilikuwa baina ya APR na Rayon Sports. Katika dakika za kawaida timu hizi zilitoka sare ya mabao 2-2.
Katika hatua ya nusu fainali mechi zote mbili zilifikia hatua ya mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukomaa ndani ya dakika 120.
Baada ya yote, APR dhidi ya El Merreikh watakutana kesho jumapili katika mchezo wa fainali utakaopigwa uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
Mechi hii inatarajia kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote.

Timu zote zimesheheni vijana wadogo wenye vipaji vya hali ya juu, hivyo kandanda safi linatarajiwa katika dimba hilo la Amahoro ambalo maana yake ni Amani.

waliotembelea blog